Jan 15, 2022 07:29 UTC
  • Marekani yajipanga kutumia meli zisizo na nahodha katika eneo la Asia Magharibi

Kamanda wa manowari ya tano ya Marekani (FIFTH Fleet), kikosi hicho kinalenga kupanua wigo wa utumiaji meli zisizo na nahodha na zinazojiendesha zenyewe katika eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati).

Brad Cooper amesema, jeshi la majini la Marekani linajiandaa kutumia meli zisizo na nahodha katika eneo la Asia Magharibi kwa ajili ya kuifanyia kazi teknolojia na kuitayarishia mazingira mapya ya kiutendaji kamandi kuu ya kijeshi ya nchi hiyo CENTCOM.

Kamanda huyo wa manowari ya tano ya Marekani amebainisha kuwa, mazoezi ya 22 kimataifa ya vikosi vya majini yatajikita kwenye manuwari maalumu ya meli zisizo na nahodha ambazo zilitumiwa katika manowari hiyo ya tano mwezi Septemba mwaka jana.

Brad Cooper

Kwa mujibu wa Cooper, nchi 60 zitashiriki katika mazoezi hayo ya kijeshi ya 22 na akaongeza kuwa, nchi kumi washiriki kati ya hizo zitatumia meli zisizo na nahodha katika manuva hayo.

Manuwari ya tano ya Marekani ambayo makao yake yako nchini Bahrain ilitangaza mwezi uliopita kuwa imeunda kikosi kipya katika Ghuba ya Uajemi cha kuunganisha ndege zisizo na rubani na meli zisizo na nahodha ambazo zitaongozwa katika operesheni zake na mfumo wa akili bandia. 

Marekani inachukua hatua hiyo katika hali ambayo, kuwepo kwake kijeshi pamoja na baadhi ya madola mengine ya nje ya eneo na kuigeuza Ghuba ya Uajemi ghala la silaha zao, kumechochea na kushamirisha machafuko na ukosefu wa usalama katika eneo hili.../