Jan 19, 2022 11:02 UTC
  • Rais wa Iran awasili Moscow kwa ziara rasmi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewasili Moscow, mjii mkuu wa Russia hii leo Jumatano ikiwa ni katika kujibu mwaliko wa rais wa nchi hiyo Vladimir Putin.

Mara tu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moscow, Rais Ebrahim Raisi wa Iran na ujumbe anaoandamana nao walilakiwa na Nikolai Shulginov, Waziri wa Nishati wa Russia ambaye pia ni mkuu wa kamisheni ya pamoja ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi mbili.

Katika sherehe ya mapokezi, mara tu baada ya kuimbwa nyimba za mataifa mawili ya Iran na Russia, Rais Raisi alikagua gwaride ya heshima iliyoandaliwa kwa ajili yake.

Katika safari hiyo mbali na kuzungumza na mwenyeji wake Rais Vladimr Putin, Rais Raisi pia atakutana na viongozi, jumuia na jumbe mbalimbali zikiwemo za raia wa Iran wanaoishi na kufanya kazi nchini Russia.

Marais Putin wa Russia (kushoto) na Raisi wa Iran

Rais Ebrahim Raisi anayeoongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Iran amefanya safari nchini Russia kufuatia mwaliko aliopewa na Rais Putin.

Mawaziri wa mambo ya nje, mafuta na uchumi na masuala ya fedha ni miongozi mwa viongozi wa ngazi za juu wanaoandamana na Rais Raisi katika safari hiyo.

Ikiwa ni katika siasa za serikali yake za kuimarisha ushirikiano na nchi jirani na za eneo, Rais Raisi tayari amekwishafanya safari kama hiyo katika nchi za Tajikistan na Turkemanistan.