Jan 22, 2022 08:08 UTC
  •  Antonio Guterres
    Antonio Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulizi ya ndege za kivita za Saudi Arabia dhidi ya jela ya wafungwa katika mkoa wa Sa'ada nchini Yemen.

Taarifa iliyotolewa na Antonio Guterres imesema shambulizi jingine limesajiliwa nchini Yemen  ambalo limeua raia wakiwemo watoto wadogo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka na wa wazi kuhusu mashambulizi hayo na kuwawajibishwa wahusika.

Vilevile ametoa wito wa kukomeshwa mzingiro wa Saudia na washirika wake dhidi ya bandari na viwanja vya ndege vya Yemen na kuanzishwa tena mazungumzo ya kutafuta suluhisho la mgogoro wa nchi hiyo. 

Hata Waislamu miskitini hawakusalimika na mashambulizi ya Saudia huko Yemen

Mashambulizi ya anga yaliyofanywa na ndege za kivita za Saudia dhidi ya jela ya mkoa wa Sa'ada huko Yemen yametajwa kuwa miongoni mwa mashambulizi yaliyosababisha maafa makubwa ya raia.

Takwimu za karibuni zinasema watu wasiopungua 77 wameuawa katika hujuma hiyo ya kinyama ya ndege za kivita za utawala wa kifalme wa Saudi Arabia na wengine zaidi ya 140 wamejeruhiwa. 

Tags