Jan 24, 2022 03:12 UTC
  • WHO: Omicron huwenda ikahitimisha corona barani Ulaya

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani barani Ulaya ameeleza kuwa maambukizi ya kirusi cha corona aina ya Omicron huwenda yakawa mwisho wa kumalizika ugonjwa wa UVIKO-19 barani Ulaya.

Dakta Hans Kluge ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani katika ofisi ya shirika hilo barani Ulaya jana Jumapili amebainisha kuwa, maambukizi ya kirusi cha corona aina ya Omicron yamepelekea maambukizi ya corona kuingia katika marhala mpya na kwamba kuna uwezekano maambukizi hayo yakahitimisha maradhi ya Uviko-19 barani Ulaya. Dakta Kluge amaeshiria namna kirusi cha Omicron hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu kitakuwa kimeambukiza asilimia 60 ya jamii ya watu wa Ulaya na kuongeza kuwa: upo uwezekano kwamba ukanda wa Ulaya unaelekea kuhitimisha maambukizi ya corona. 

Omicron huwenda ikahimitisha corona barani Ulaya 

Kirusi hicho cha corona aina ya Omicron ambacho utafiti unaonyesha kuwa kiujumla madhara yake ni ya kiwango cha chini ikilinganishwa na kile cha Delta kimetoa matarajio haya kwamba,  corona ni  ugonjwa unaobadilika na kuweza kukabiliana nao sawa kabisa na homa ya mafua ya infuluenza.  

Shirika la Afya Duniani (WHO) pia hivi karibuni lilitangaza kuwa, zaidi ya nusu ya jamii ya watu wa Ulaya watapata maambukizi ya kirusi cha corona aina ya Omicron katika muda wa miezi miwili ijayo iwapo maambukizi ya sasa ya Omicron yataendelea.

 

Tags