Jan 26, 2022 04:14 UTC
  • Mgombea urais Ufaransa kupiga marufuku majina ya

Mgombea mwenye siasa kali za mrengo wa kulia katika uchaguzi wa rais wa Ufaransa, Éric Zemmour, ametangaza ajenda na mipango yake kuhusu dini ya Kiislamu, ambayo amesema ataitekeleza iwapo ataingia Ikulu ya Elysee.

Sera na mipango ya Éric Zemmour iliyochapisha kwenye akaunti yake ya Twitter, inajumuisha marufuku ya uvaaji wa nguo zote zenye alama za Kiislamu - ikiwa ni pamoja na vazi la hijabu - katika viwanja vya umma, pamoja na marufuku ya kujenga minara na misikiti nchini Ufaransa.

Katika mahojiano yake ya hapo awali ya televisheni, Zammour alisema kuwa atawazuia Waislamu nchini Ufaransa kuwapa watoto wao jina la "Muhammad" endapo atashinda kiti cha Rais wa Jamhuri, na kuongeza kuwa ataweka jedwali la majina wanayopewa watoto wa Kiislamu.

Watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekosoa misimamo hiyo ya mgombea urais wa Ufaransa wakisema kwamba Zemmour amefikia hatua ya hatari ambayo yumkini ikamsukuma kuanzisha vita dhidi ya Waislamu nchini Ufaransa, na kuwafukuza nchini humo.

Le Pen na Zemmour

Éric Zemmour anachuana na kiongozi wa chama cha National Rally Party, Marine Le Pen, 53, katika kuwania uongozi wa mrengo wa kulia wenye siasa kali nchini Ufaransa, na baadhi ya uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa, amempiku na kuwa mpinzani mkuu wa Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, katika uchaguzi ujao wa rais.

Mamepa mwezi huu Éric Zemmour alitozwa faini ya Euro 10,000 na Mahakama ya Paris kwa kupatikana na hatia ya kutoa matamshi ya chuki na ya kibaguzi. 

Kesi hiyo ilifunguliwa baada ya kusema katika kipindi cha televisheni kuwa, watoto wahamiaji wasioandamana na wazazi wao ni "wezi", "wabakaji" na "wauaji".

Zemmour anajulikana kwa mitazamo yake ya chuki dhidi ya Uislamu na wahamiaji.

Tags