Jan 28, 2022 06:50 UTC
  • Dmitry Polyanskiy
    Dmitry Polyanskiy

Naibu mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuondoka mara moja wanajeshi wote wa kigeni walioko nchini Syria.

Dmitry Polyanskiy amekosoa uwepo wa wanajeshi wa Marekani nchini Syria bila ya kusaidia mapambana dhidi ya ugaidi na kusisitiza kuwa Russia itaendeleza jitihada zake za kukabiliana na ugaidi nchini Syria.

Ameongeza kuwa, "Marekani haipigani na ugaidi, si kikanda wala katika upeo wa kimataifa."

Wakati huo huo  Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa, ndege za kivita za nchi hiyo na Syria zinashika doria kwa pamoja katika anga ya mipaka wa Syria, ikiwemo milima ya Golan.

Wapiganaji wa kundi la Kikurdi la Syrian Democratic Forces (SDF) lenye mfungamano na Marekani na wanamgambo wanaoungwa mkono na jeshi la Uturuki, wamevamia kinyume cha sheria maeneo ya kaskazini na kaskazini mashariki mwa Syria ambako mbali na kupora rasilimali za mafuta ya nchi hiyo, wanafanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya wakaazi ya raia wa maeneo hayo na vikosi vya jeshi la Syria.

Maafisa wa Syria wanasisitiza kwamba, kuwepo kwa majeshi ya Marekani na washirika wake katika ardhi ya nchi hiyo ni uvamizi. Marekani ndiyo mfadhili na muungaji mkono mkuu wa makundi ya kigaidi yanayopigana dhidi ya serikali halali ya Syria. 

Tags