Apr 02, 2022 07:50 UTC
  • Chanjo ya kwanza ya COVID-19 kwa njia ya pua duniani yasajiliwa Russia

Wizara ya Afya ya Russia imesajili chanzo ya kwanza duniani ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 inayotolewa kupitia puani.

Kirusi cha corona kiligunduliwa kwa mara ya kwanza mwezi Disemba mwaka 2019 katika mji wa Wuhan huko China. Hadi sasa watu zaidi ya milioni 490 wameambukizwa kirusi hicho angamizi na wengine zaidi ya milioni 6 na 171,000 wameaga dunia kwa COVID-19.  

Shirika la habari la Sputnik limeripoti kuwa, Idara ya Mawasiliano katika Wizara ya Afya ya Russia imetangaza kuwa, wizara hiyo imesajili  chanjo ya   COVID-19 kwa jina la Gam-COVID-Vac (Sputnik V) itayotolewa kupitia puani. Chanjo hiyo ya corona imetengenezwa na Taasisi ya  Utafiti wa Vijidudu Maradhi ya Gamaleya ya  Russia ili kuzuia maambukzi mapya ya corona. 

Chanjo hiyo imetengenezwa kwa kutumia mada za aina mbili na hupulizwa ndani ya pua ya mgonjwa kwa wiki tatu. Wizara ya Afya ya Russia imesema kuwa chanjo hiyo inaruhusiwa kupewa watu walio na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.  

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Vijidudu Maradhi ya Gamaleya ya  Russia, Alexander Giznburg alisema mwezi huu kuwa, wanasayansi wamebaini kuwa chanjo ya Gam-COVID-Vac ina uwezo wa kukabiliana na maambukizi ya spishi aina ya Omicron kutokana na majaribio yaliyofanywa puani kwa kutumia chanjo hiyo.

Chanjo ya puani ya Russia inafaa kwa spishi ya Omicron 

 

Tags