Apr 02, 2022 12:59 UTC
  • Nchi za Ulaya zasajili rekodi mpya ya mfumko wa bei za bidhaa

Mfumko wa bei za bidhaa katika nchi za bara Ulaya ulikwea hadi kiwango cha kutisha cha asilimia 7.5 mwezi uliopita wa Machi.

Ofisi ya Takwimu ya Umoja wa Ulaya imesema mfumko wa bei za bidhaa katika nchi za eneo la Ulaya ulifikia asilimia 44.7 mwezi Machi, ikilinganishwa na asilimia 32 mwezi Februari.

Kuongezeka kwa bei za nishati mwaka hadi mwaka kumeripotiwa kuwa moja ya sababu kuu za nchi za Ulaya kushuhudia mfumko wa bei za bidhaa ambao haujawahi kushuhudiwa tena katika miongo ya hivi karibuni.

Ripoti ya Ofisi ya Takwimu ya EU inaonyesha kuwa, bei za chakula, pombe na bidhaa za tumbaku zilipanda kwa asilimia 5 mwezi Machi mwaka huu katika nchi za bara Ulaya, ikilinaginishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Nchi za Ulaya zilizosajili kiwango kikubwa cha mfumko wa bei za bidhaa mwezi Machi mwaka huu ni pamoja na Lithuania, asilimia 15.6, Estonia, asilimia 14.8 na Uholanzi asilimia 11.9.

Wachumi wameonya kuwa, chumi za nchi za Ulaya zinaelekea kushuhudia kipindi kigumu zaidi mwezi huu wa Aprili, kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu, kulikosababishwa na mgogoro wa Ukraine. 

Bert Colijn, mchumi mwandamizi wa shirika la ING amesema si muhali mfumko wa bei za bidhaa katika eneo la Ulaya ukapindukia hata asilimia 10, kutokana na bei za juu za nishati, na kuvurugwa kwa usambazaji wa bidhaa kutokana na operesheni ya kijeshi ya Russia nchini Ukraine.

Tags