Apr 04, 2022 07:37 UTC
  • Kwa mara ya kwanza katika historia: Bunge la Pakistan latoa nara ya

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Bunge la Pakistan, wabunge wa nchi hiyo wametoa nara ya "Kifo kwa Marekani" huku bunge hilo likipinga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, iliyotaka kumuondoa madarakani Imran Khan, ambaye ameyatuhumu madola ya kigeni kuwa yanaingilia demokrasia ya nchi hiyo.

Qasim Khan Suri, Naibu Spika wa Bunge la Taifa la Pakistan, alipuuzilia mbali wito wa kutokuwa na imani na waziri mkuu siku ya Jumapili, na kuitaja kuwa "inapingana" na Kifungu cha 5 cha Katiba ya Pakistan.

Suri alisema kuwa hoja hiyo iliyowasilishwa Machi 8 inapaswa kufuata sheria na Katiba, akisisitiza: "Hakuna mamlaka ya kigeni itakayoruhusiwa kupindua serikali iliyochaguliwa na wananchi."

Baada ya wabunge wa Pakistan kukataa hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Rais wa nchi hiyo alichukua hatua ya kulivunja Bunge kwa ushauri wa Imran Khan.

“Rais wa Pakistan, Dk Arif Alvi, ameidhinisha ushauri wa Waziri Mkuu,” imesema taarifa kutoka Ofisi ya Rais, ikimaanisha kwamba uchaguzi mpya wa Bunge unapaswa kufanyika ndani ya siku 90.

Upinzani umeapa kupinga hatua hiyo katika Mahakama ya Juu ya Pakistan.

Jumamosi iliyopita Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan aliishutumu Marekani kwa kuchochea mjadala wa Bunge kuhusu hoja ya kutokuwa na imani naye, akisema hatua hiyo ni jaribio la kubadilisha utawala linaloungwa mkono na Washington.

Imran Khan

Imran Khan anaamini kuwa mashinikizo ya vyama vya upinzani yanayomtaka ajiuzulu yanatokana na njama za nchi za kigeni kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali yake kutokana msimamo wake usioyumba kuhusu siasa zake za nje na ndani ya nchi.

Tags