Apr 23, 2022 12:23 UTC
  • Uchunguzi wa maoni: Macron atashinda uchaguzi wa rais Ufaransa

Matokeo ya uchunguzi wa maoni kuhusu duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Ufaransa yaliyochapishwa hadi kumalizika kwa muda wa kisheria wa kampeni za wagombea wawili wa uchaguzi huo yameonesha kuwa Emmanel Macron atashinda kiti cha rais.

Wafaransa wa Jumapili ya kesho watamchagua mmoja kati ya wagombea wawili; Emmanuel Macron na Marine Le Pen, mgombea wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa miaka mitano. Muda wa kisheria ya kampeni za wagombea urais wa Ufaransa umekamilika usiku wa manane wa kuamkia leo, na matokeo ya uchaguzi hayatachapishwa hadi kesho usiku, wakati matokeo ya awali ya uchaguzi huo yatakapotangazwa.

Uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni nchini Ufaransa unaonesha kuwa Emmnuel Macron atashinda uchaguzi huo kwa tofauti ya takriban asilimia 10 hadi 15 ya kura.

Makadirio yanaonesha kuwa, Marine Le Pen atapata asilimia 42.5 hadi 44.5 ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi na Macron atapata asilimia 55.5 hadi 57.5.

Mchambuzi wa kituo cha uchunguzi wa maoni  cha Elabe Opinion amesema Le Pen atapata asilimia 44.5 ya kura, na Emmanuel Macron asilimia 55.5.

Macron na Le Pen

Ripoti ya kituo cha uchunguzi wa maoni cha Ifop pia inaonesha kuwa Macron atashinda uchaguzi kwa tofauti ya asilimia 10 ya kura.

Wakti huo huo uchunguzi wa maoni umebaini kuwa asilimia 14 ya Wafaransa wanaamini kuwa kuna uwezekano wa wizi wa kura na udaganyifu katika uchuguzi huo.

Gazeti la Le Figaro limeandika kuwa, uchunguzi uliofanywa na taasisi ya IFOP umebaini kuwa asilimia 14 ya Wafaransa wanaamini kuwa duru ya pili ya uchaguzi itakumbwa na wizi wa kura. 

Tags