May 06, 2022 12:31 UTC
  • Seneta Rand Paul: Marekani ni kinara wa kusambaza habari za uongo duniani

Seneta wa chama cha Republican, Rand Paul amesema serikali ya Marekani ndiyo kinara wa kueneza habari za uongo katika historia ya dunia.

Rand Paul amesema kwamba serikali iliyozoea kusema uwongo ya Marekani haina haki ya kuwaambia watu wake nini "ukweli" na si kweli kwa sababu ndiyo kinara wa kusambaza habari za uongo.

Matamshi hayo ya seneta Rand Paul yametolewa baada ya Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani, Alejandro Nicholas Mayorkas kutetea hoja ya kuundwa "bodi ya uongo" katika kikao cha Baraza la Seneti na kudai kuwa, mitandao ya kijamii imesaidiwa sana kuchuja "habari bandia".

Akijibu matamshi ya waziri huyo, Rand Paul ameashiria uongo mwingi wa serikali ya Marekani, akisema kuwa serikali ya nchi hiyo imekuwa ikiwadanganya wananchi kwa miaka mingi kuhusu Vita vya Vietnam.

Rand Paul pia ameashiria uongo wa George W. Bush", rais wa zamani wa Marekani kuhusu kuwepo "silaha za maangamizi ya umati nchini Iraq" uliotumiwa kama kisingizio cha uvamizi wa Marekani na kuikalia kwa mabavu Iraq kwa kipindi cha miongo miwili.

Seneta huyo amemwambia Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani kwamba: "Hivi unadhani kuwa watu wa Marekani ni wajinga sana kiasi cha kuwaambia nini kweli na si kweli?"

Mwishoni mwa mwezi uliopita, serikali ya Marekani ilitangaza kuunda bodi ya kusimamia habari za uongo ili kukabiliana na usambazaji wa taarifa za uongo nchini humo.

Hatua hiyo imekosolewa na wanasiasa na vyombo vya habari. 

Tags