May 16, 2022 07:33 UTC
  • Mashauriano ya Blinken na Troika ya Ulaya kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA

Akizungumza karibuni kando ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameshauriana na mawaziri wenzake wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza kuhusu mapatano ya nyuklia ya Iran na vilevile matukio ya hivi karibuni nchini Ukraine.

Akizungumza hapo jana Jumapili na mawaziri wenzake wa  Umoja wa Ulaya (Ujerumani, Ufaransa na Uingereza) kando ya mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO mjini Berlin, Anthony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amejadiliana na wenzake hao kuhusu hali ya Ukraine na mazungumzo ya Vienna kuhusu kuondolewa vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Blinken ameeleza kuwa amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalla Bayerbauk, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Elizabeth Terrace na Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kisiasa na Usalama wa Ufaransa Philippe Sachs ambapo wamejadili mipango ya kuendelea kuiunga mkono Ukraine na kumchukulia Rais Vladimir Putin wa Russia kuwa muhusika mkuu wa uvamizi dhidi ya Ukraine.

Hapo awali, Blinken pia alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmitry Kolba na kujadiliana naye kuhusu usalama na usaidizi wa kiuchumi wa nchi za Magharibi kwa Kiev.

Viongozi wa Marekani wakiwachochea viongozi wa Ukraine dhidi ya Russia

Katika upande mwingine, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa, kwa kuzingatia kuwa Marekani ndio mkiukaji mkuu wa makubaliano JCPOA, ni Washington ndiyo inapaswa kurejea katika mapatano hayo kwa kuondoa vikwazo na kutekeleza wajibu kwenye mapatano hayo. Tehran inasisitiza kuwa haina haraka ya kuona Marekani ikilazimishwa kurejea kwenye makubaliano hayo.

Russia ilianzisha operesheni ya kijeshi nchini Ukraine mnamo tarehe 24 Februari kufuatia hatua za uchochezi za NATO kwenye mpaka wake, na nchi za Magharibi, haswa Marekani, sio tu kwamba zimekataa kupunguza mvutano na kumaliza mzozo wa Ukraine, bali zenyewe zimekuwa zikichangia pakubwa kuongezeka mgogoro huo kwa kutuma nchini humo kila aina ya silaha za kisasa na zana za kijeshi na wakati huo huo kutoa mashinikizo makubwa dhidi ya Russia.

Tags