May 16, 2022 10:45 UTC
  • Asilimia 75 ya Wamarekani wanaona nchi yao inaenda upande sio; Ukraine imechangia

Uchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni unaonesha kuwa, umaarufu wa rais wa Marekani, Joe Biden umeporomoka tena, huku asilimia 75 ya Wamarekani wakiamini kuwa nchi yao inaendeshwa ovyo.

Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni uliofanya na televisheni ya NBC News ya Marekani yanaonesha kuwa, mwezi Septemba 2021 umaarufu wa Joe Biden ulikuwa baina ya asiliia 40 hadi 43 lakini hivi sasa umeporoka vibaya tangu alipoingia madarakani.

Matokeo hayo yanaonesha kuwa, asiliimia 56 ya walioshiriki kwenye uchunguzi huo wamesisitiza kuwa, hawaridhishwi na siasa zinazoendeshwa na Joe Biden huku asilimia 75 ya Wamarekani hao wamesema wazi kuwa nchi yao inapelekwa upande sio.

Siasa za serikali ya Biden za kutumia fedha nyingi kwa ajili ya Ukraine, kupata kwa gharama za maisha hasa baada ya serikali ya Joe Biden kutangaza vikwazo dhidi ya Russia, suala zima la ugonjwa wa corona zimetajwa kuwa ni miongoni mwa kuporomoka umaarufu wa Biden kati ya wananchi wa Marekani.

Siasa mbovu na matumizi ya ovyo ya fedha za taifa yameifikisha hapa Marekani

 

Matokeo ya uchunguzi mwingine wa maoni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Monmouth cha Illinois yanaonesha kuwa, kiwango cha umaarufu wa Joe Biden hivi sasa kimeporomoka na kufikia kama cha rais aliyemtangulia, Donald Trump katika muda kama huo.

Baraza la Wawakilishi la Marekani hivi karibuni limepasisha msaada wa takriban dola bilioni 40 kwa Ukraine na kupeleka muswada huo kwa Baraza la Sanate la nchi hiyo. Iwapo muswada huo utapasishwa na Baraza la Sanate, kitakachobakia ni kutiwa saini tu na Joe Biden ili uwe sheria.

Matumizi ya kiholela ya fedha za taifa huko Marekani yanafanyika katika hali ambayo, mgogoro wa kupanda bei ya mafuta unaendelea kuvunja rekodi nchini humo na hivi sasa bei ya bidhaa hiyo muhimu imevunja rekodi ya historia nzima ya Marekani.

Tags