May 17, 2022 11:24 UTC
  • Taliban: Hatuna uadui wowote na Marekani, tunafirikia kuanzisha nayo uhusiano mzuri

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Taliban Sirajuddin Haqqani amesisitiza kuwa, kwa sasa, serikali ya Afghanistan si tu haiitazami Marekani kama adui, bali inafikria pia kuanzisha uhusiano mzuri na Washington.

Sisitizo hilo la Haqqani lenye madhumuni maalumu, la kwamba Taliban haina uadui na Marekani na kuunga mkono kuwa na uhusiano imara na Washington, limetolewa katika hali ambayo, jina la waziri huyo wa mambo ya ndani wa serikali ya Taliban lingaliko kwenye orodha ya magaidi ya vyombo vya usalama vya Marekani. Isitoshe, si Taliban pekee, bali wananchi wote wa Afghanistan wanaitambua Marekani kama adui nambari moja wa nchi yao kwa kuitambua Washington kama msababishaji mkuu wa matatizo yanayoikabili hivi sasa Afghanistan kutokana na kuzuia fedha na mali za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Sauti ya Afghanistan, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Taliban Sirajuddin Haqqani ameiambia televisheni ya CNN: "kwa sasa hatuitazami Marekani kama adui na tunataka katika mustakabali tuwe na uhusiano mzuri na Marekani na jamii ya kimataifa kulingana na sheria na misingi inayotawala katika sehemu zingine za dunia."

Hii ni katika hali ambayo, Polisi ya Upelelezi ya Serikali Kuu ya Marekani FBI imetenga kitita cha dola milioni 10 kwa ajili ya kumkamata au kumuua Haqqani.

Hapo kabla, Sirajuddin Haqqani alikuwa akikwepa kushiriki katika vikao rasmi, akiziba sura yake na kubeba silaha katika vikao vya hadhara; lakini kuanzia kitambo kifupi nyuma hadi sasa amekuwa akijitokeza na kuonekana hadharani.../ 

Tags