May 19, 2022 07:11 UTC
  • Benki ya Dunia yatenga dola bilioni 30 kukabili mgogoro wa chakula uliosababishwa na vita vya Ukraine

Benki ya Dunia imetangaza kuwa, imetenga dola bilioni 30 za misaada kwa ajili ya kudhibiti mgogoro wa chakula duniani uliosababishwa na vita vya Ukraine.

Shirika la habari la IRNA limeripoti hayo leo Alkhamisi na kuongeza kuwa, Benki ya Dunia imetangaza kwamba misaada hiyo itajumuisha dola bilioni 12 za kuendesha miradi mipya na zaidi ya dola bilioni 18 za kuendeleza na kukamilisha miradi iliyopo ya kudhamini chakula.

Benki hiyo ya dunia aidha imesema, miradi mipya itaekezwa kwenye kilimo, kukabiliana na athari za kuongezeka bei za vyakula kwa watu maskini na miradi ya maji na kilimo cha umwagiliaji.

Benki ya Dunia

 

Misaada hiyo mingi itatolewa kwa nchi za Afrika, nchi za Asia Magharibi, Ulaya Mashariki, Asia ya Kati na Asia Kusini, maeneo ambayo ndiyo yaliyoathiriwa zaidi na vita vya Ukraine.

Hayo yameripotiwa katika hali ambayo mgogoro wa kupanda bei ya mafuta unaendelea kuvunja rekodi nchin Marekani na hivi sasa bei ya bidhaa hiyo muhimu imevunja rekodi ya historia nzima ya nchi hiyo.

Mgogoro wa nishati ni mkubwa Marekani kiasi kwamba, taarifa za kuaminika kutoka vyanzo vitatu zinasema kuwa, mwezi Machi mwaka huu, viongozi wa Marekani waliiomba Brazil iongeze kiwango cha uzalishaji mafuta yake na kuingiza katika soko la dunia, lakini serikali ya nchi hiyo ililipiga na chini ombi hilo la Marekani.

Hayo yamekuja baada ya uUchunguzi wa karibuni kabisa wa maoni kuonesha kuwa, asilimia 75 ya Wamarekani wanaaamini kuwa nchi yao inaendeshwa ovyo has katika kadhia ya Ukraine na kuiwekea kwake vikwazo Russia.