May 21, 2022 12:29 UTC
  • Wanaharakati wa asasi za kiraia Korea Kusini waandamana kupinga safari ya Biden

Baadhi ya wanaharakati wa asasi mashuhuri za kiraia nchini Korea Kusini wamekusanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Seoul kupinga safari ya Rais Joe Biden wa Marekani nchini humo.

Biden alianza rasmi safari yake ya siku sita ya kaskazinimashariki ya Asia hapo jana Ijumaa Mei 20, ambapo ndege iliyombeba rais huyo wa Marekani ilitua katika kituo cha kwanza ziara yake cha Korea Kusini.

Shirika la habari la IRIB limeripoti kuwa, wapinzani wa safari ya rais wa Marekani nchini Korea Kusini walimiminika mabarabarani wakiwa wamebeba maberamu yaliyoandikwa nara na kaulimbiu tofauti ikiwemo "safari ya Biden Korea Kusini inashadidisha mgogoro wa vita", "tunapinga serikali ya Yoon Seok-youl kujiingiza kwenye vita vipya baridi vya Marekani" na "tunapinga ushirikiano wa kijeshi wa Japan na Korea Kusini."

Yoon na Biden

Wanaharakati hao wamesisitiza kuwa, sera kuu inayofuatwa na serikali ya Korea Kusini ya kuimarishwa umoja na ushirikiano wa kijeshi baina ya Marekani na nchi hiyo na kushamirisha pia mashirikiano ya kijeshi ya pande tatu kati ya Marekani, Japan na Korea Kusini, sambamba na stratejia ya uhasama wa kijeshi inayofuatwa na Washington, vinaifanya hali ya mambo katika Peninsula ya Korea iwe mbaya zaidi na kuzidisha mivutano na mashindano ya silaha katika eneo hilo.

Waandamanaji hao wameitaka serikali ya Seoul ichague na kufuata njia ya suluhu, amani na ushirikiano.../

Tags