May 26, 2022 07:46 UTC
  • Seneta Murphy: Kununua silaha Marekani ni rahisi kuliko kununua mnyama wa kufuga

Seneta wa chama cha Republican amekiri kwamba, kununua silaha nchini Marekani ni rahisi mno kuliko hata kununua mnyama wa kufuga.

Seneta Chris Murphy amekosoa vikali sheria nyepesi nchini Marekani zinazorahisisha kununua na kumiliki silaha.

Akizungumza kufuatia tukio la kuuawa wanafunzi 19 katika tukio la kusikitisha la ufyatuaji risasi huko Texas Marekani, Seneta huyo amesema, usalama wa kiakili na kisaikolojia siyo sababu pekee ya matukio ya ufyatuaji risasi na mauaji katika shule za nchi hiyo bali upatikanajii kirahisi na umiliki kiholela wa silaha nchini humo ni jambo ambalo limekuwa na taathira kubwa katika matukio ya mauaji na ufyatuaji risasi katika skuli za Marekani.

Amesema, wakati wananchi wa Marekani wanapokuwa na fikra ya kuua watu wengine, huweza kwenda dukani na kununua silaha kwa urahisi kabisa huku sheria za kununua wanyama wa kufuga majumbani zikiwa kali zaidi kuliko sheria za kumiliki silaha.

Seneta Chris Murphy

 

Watoto wadogo wasiopungua 19 waliuawa kwa umati baada ya gaidi mmoja aliyetajwa kwa jina la Salvador Ramos kuvamia shule yao huko Uvalde Texas Marekani juzi Jumanne.

Mauaji ya umati na ya kiholela ni jambo la kawaida sana nchini Marekani. Televisheni ya CNN imetangaza kuwa, mwaka 2020 jimbo la Mississippi ambalo sheria za kubeba silaha moto ni nyepesi mno, ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya watu waliouawa kwa silaha hizo.