Jun 26, 2022 07:44 UTC
  • Putin atangaza kutumwa kwa makombora ya Alexander huko Belarusi

Rais wa Russia, Vladimir Putin alitangaza jana katika mazungumzo yake na rais mwenzake wa Belarus, Alexander Lukashenko huko St. Petersburg kwamba Moscow inapeleka mifumo ya makombora ya Iskander-M huko Belarus.

Putin amesema: "Moscow itatuma mifumo hii ya kisasa ya makombora huko Belarusi katika miezi michache ijayo."

Bwana Lukashenko alisema katika mazungumzo hayo kwamba: "Tuna wasiwasi na sera za uchokozi za majirani zetu, Lithuania na Poland."

Ametoa wito kwa Putin kuisaidia nchi hiyo katika kukabiliana na Jumuiya ya Kijeshi ya Nchi za Magharibi (NATO) na kuzipa ndege za Belarus uwezo wa kubeba makombora ya nyuklia.

Rais Vladimir Putin na Alexander Lukashenko 

Hata hivyo Rais Vladimir Putin amesema: "Kwa sasa hakuna haja ya kuchukua hatua dhidi ya NATO na washirika wake, lakini ndege za Sukhoi 25 zinaweza kuongezwa kwenye kikosi cha anga cha Belarus."

Mbali na kutuma mifumo ya makombora ya Iskander-M, Putin pia ameahidi kuipatia Belarus mfumo mwingine wa makombora ya kisasa.

Russia na washirika wake wanapinga sera za Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO za kujipanua upande wa Mashariki. 

Tags