Jun 27, 2022 03:58 UTC
  • New York Times yafichua shughuli za siri za CIA na kikosi maalumu cha Marekani  Ukraine

Gazeti la New York Times linalochapishwa nchini Marekani limefichua kuhusu harakati za siri zinazofanywa na Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA) na kikosi maalumu cha wanajeshi wa nchi hiyo huko Ukraine.

New York Times limefichua kuwa kanali ya siri ya majasusi wa CIA na kikosi maalumu cha wanajeshi wa Marekani na nchi waitifaki dhidi ya Russia wanalisaidia jeshi la Ukraine. 

Likiendelea kufichua kuhusu misaada inayotolewa na kanali za siri na za kijasusi za nchi za Magharibi kwa Ukraine dhidi ya Russia, gazeti la New York Times limeandika kwamba akthari ya jitihada za nchi za Magharibi za kuisaidia Ukraine zinatekelezwa nje ya nchi hiyo; kwa mfano katika kambi za kijeshi huko Ujerumani, Ufaransa na Uingereza.  

Nchi za Magharibi hasa Marekani zinaipatia Ukraine silaha na zana mbalimbali za kijeshi na kuzidisha mashinikizo kwa Russia tangu kuanza vita huko Ukraine, huku vita na mzozo vikishaididi ndani ya Ukraine. 

Kikosi maalumu cha wanajeshi wa Marekani nchini Ukraine

Russia aidha imetahadharisha kuwa, silaha na zana za kivita zinazotolewa na Marekani na Ulaya kwa Ukraine zinashadidisha tu mzozo nchini humo na kusabababisha maafa yasiyotabirika. Ni zaidi ya miezi minne sasa ambapo Ukraine imeathiriwa na vita ambavyo Russia ilivianzisha lengo likiwa ni kuipokonya silaha Ukraine na kujibu ombi la viongozi wa maeneo ya Donetsk na Luhansk. 

Tags