Jun 27, 2022 07:53 UTC
  • Uingereza yatangazwa kuwa 'makao makuu' ya utapeli duniani

Gazeti la Daily Mail limeeleza katika ripoti kuwa, kila mwaka hufanywa utapeli wa paundi bilioni tatu nchini Uingereza ambao umeigeuza nchi hiyo kuwa makao makuu ya uhalifu na utapeli duniani.

Utafiti uliofanywa na gazeti hilo unaonyesha kuwa, wimbi jipya na la kutisha la utapeli nchini Uingereza limepelekea kuibiwa paundi milioni mia saba katika mwezi Aprili mwaka huu. 

Hayo yanajiri wakati mwaka uliopita, katika kila mwezi ulifanyika utapeli kwa wastani wa paundi milioni mbili nchini Uingereza.

Halikadhalika Daily Mail limetangaza kuwa, katika mwaka huu Waingereza milioni 40 wametapeliwa; ni tukio moja tu kati ya kila matukio saba ya utapeli liliripotiwa polisi; na polisi ya Uingereza imefanya uchunguzi wa asilimia mbili tu ya ripoti za matukio yote ya utapeli yaliyoripotiwa.

Image Caption

 

Wakati huohuo shirika la usalama wa kimtandao la Uingereza limeripoti kuwa, katika mwaka uliopita lilizima hujuma milioni mbili na laki saba za utapeli kupitia mitandao ya intaneti, likiwa ni ongezeko mara nne kulinganisha na mwaka wa kabla yake wa 2020.

Katika upande mwingine, kituo cha taifa cha usalama wa mitandao ya intaneti kinachofanya kazi chini ya tume ya serikali ya Uingereza kimetangaza kuwa, matukio ya utapeli yaliyonaswa na kubainika ni pamoja na hati za kuidhinisha mambo kwa kutumia majina ya watu mashuhuri, baruapepe bandia na uchukuaji rubuni kwa vitisho kwa wahanga wa utapeli.

Kwa mujibu wa kituo hicho, janga la corona limechangia kuongezeka matukio ya utapeli uliohusisha shriika la afya la nchi hiyo.../