Jun 28, 2022 07:59 UTC
  • Sakata; Biden ametumia fedha nyingi kugharamia ufuska wa kijana wake

Gazeti la Washington Examiner limefichua kashfa ya ufuska inayoizunguka familia ya Rais Joe Biden wa Marekani, ambapo kiongozi huyo wa Marekani anaripotiwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kugharamia ufuska wa mtoto wake wa kiume, Hunter Biden.

Gazeti hilo limenukuu data zilizopatikana kwenye kipakatakilishi (laptop) cha Hunter Biden zilizofichua kuwa, kijana huyo wa kiume wa Biden alitumia zaidi ya dola 30,000 kuwalipa makahaba wa Ulaya Mashariki.

Kwa mujibu wa ufichuzi huo, Hunter Biden alitumia kiasi hicho cha fedha kati ya Novemba mwaka 2018 na Machi mwaka 2019, kipindi ambacho Joe Biden alikuwa Naibu wa Rais na Rais wa Marekani.

Ripoti hiyo imesema, Biden alimtumia mwanawe dola 100,000 kumsaidia kugharamia ada na tozo zake za kila siku, ingawaje haijabainika iwapo rais huyo wa Marekani alifahamu au hukujua iwapo akthari ya fedha hizo zinatumika kugharamia mambo ya ufuska.

Februari mwaka 2019, mawasiliano ya arafa kati ya Hunter Biden na mwanamtindo wa Kirusi aliyejulikana kwa jina la 'Eva' yalivuja, baada ya wawili hao kuvutana kuhusu kucheleweshwa malipo ya mwanamke huyo. 

Rais Biden

Hunter aliripotiwa kuchelewa kumlipa mwanamke huyo dola 9,500, kwa ajili ya kuwa naye kwa muda wa saa 16. Mtoto huyo wa kiume wa Biden alisema ameshindwa kumlipa mwanamke huyo kwa kuwa alikuwa akitumia baruapepe yenye anuani ya Russia (.ru). 

Gazeti la Washington Examiner limeendelea kufichua kuwa, wakati ambapo Hunter Biden hakuwa anajihusisha na mambo ya ufuska, alikuwa anashiriki vikao vya Bodi ya Shirika la Nishati la Burisma la Ukraine, na kulipwa dola 50,000 kila mwezi licha ya kutokuwa na tajriba yoyote kwenye uwanja huo.

 

 

Tags