Jun 28, 2022 10:40 UTC
  • Maria Zakharova
    Maria Zakharova

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Russia amethibitisha kuwa Iran na Argentina zimetuma maombi ya kuwa wanachama katika jumuiya ya BRICS.

Maria Zakharova amethibitisha kuwa Argentina na Iran zimetuma maombi ya uwanachama katika jumuiya ya BRICS inayojumuisha Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ameongeza kuwa: "Wakati Ikulu ya Rais wa Marekani ikifikiria itakata, kupunguza na kupiga marufuku kitu gani duniani, Argentina na Iran zimetuma maombi ya uanachama katika BRICS." 

Maafisa wa mikutano ya BRICS wamesema, mada kuu ya vikao vya jumuiya hiyo ni mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu maendeleo ya kimataifa.

BRICS inawakilisha karibu nusu ya idadi ya watu duniani na inachangia sehemu kubwa ya nguvu za kiuchumi za dunia. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pekee ndiyo iliyoalikwa kutoka eneo la Asia Magharibi katika mkutano wa kilele wa BRICS Plus uliofanyika hivi karibuni nchini Afrika Kisini.

Akihutubua mkutano huo kwa njia ya video, Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alisema Iran inaweza kuwa mshirika endelevu wa kuunganisha nchi wanachama wa BRICS katika maeneo muhimu ya kupitisha nishati na masoko makubwa duniani kwa kuzingatia nafasi yake ya kipekee ya jiografia ya kisiasa na jiografia ya kiuchumi.

Tags