Jul 01, 2022 01:02 UTC
  • Uturuki yaafiki Sweden na Finland zijiunge na NATO na uwezekano wa vita vya dunia

Hatimaye, baada ya mazungumzo mengi, kumetiwa saini mapatano ya pande tatu baina ya Ankara, Stockholm na Helsinki kuhusu Finland na Sweden kujiounga na NATO. Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amethiitisha kuwa Uturuki imeafiki Sweden na Norway zijiunge na NATO.

Baada ya kuanza oparesheni za kijeshi za Russia nchini Ukraine, sambamba na kushadidi mivutano mashariki mwa Ulaya,  misuguano ya kisiasa baina ya pande hasimu imeshadidi. Katika hatua mpya kabisa, Finland na Sweden ambazo kwa muda mrefu zimekuwa hazipendelei upande wowote, zimewasilisha maombi ya kujiunga na NATO. Ingawa ombi hilo liliungwa mkono na wanachama wengine wa NATO lakini Uturuki ilikuwa na pingamizi.

Wakuu wa Uturuki wamekuwa wakizutuhumu Sweden na Finland kuwa zinaunga mkono makundi ya kigaidi hasa kundi la PKK, na kwa msingi huo Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki alikuwa ametangaza awali kuwa anapinga uanachama wa nchi hizo mbili katika muungano wa kijeshi wa NATO. Erdoğan  alisema: "Nchi waitifaki wetu hazipaswi kuleta ubaguzi miongoni mwa wanachama wa NATO na zinapaswa kutambua tishio kwa mwanachama moja ni tishio kwa wanachama wote."

Msimamo mkali wa Uturuki ulipelekea kufanyika mazungumzo kwa kimsingi kuwa Uturuki ilikuwa inasema kuwa Finland zinaunga mkono makundi ya upinzani yanayotaka kuipindua serikali ya Ankara hasa kundi la PKK ambalo Uturuki inalutambua kuwa  ni kundi la kigaidi. Bada ya kufanyika mazungumzo kuhusu hilo, hatimaye Uturuki imeafiki nchi hizo mbili zijimuike na NATO. Kwa hivyo nchi hizo za Ulaya zimekubali matakwa ya Ankara ya kushirikiana katika kupambana na makundi hayo ya kigaidi. Hivi sasa kwa kuondolewa kizingiti cha Uturuki, mchakato kamili wa kuziingiza Sweden na Finland katika NATO umeanza.

Eneo la mpaka wa Finland, Sweden na Russia

Nchi za Ulaya zinatumai kuwa, nchi hizo mbili zikiingia NATO basi muungano huo wa kijeshi utaimarika zaidi hasa katika kudhamini bajeti ya kijeshi. Katibu Mkuu wa NATO amesema: "Ili tuweze kujilinda katika dunia hii hatari, tunapaswa kuwa na bajeti ya kutosha ya kijeshi"

Kwa miaka mingi NATO imekuwa ikitaka kujipanua zaidi na hitajio hilo sasa limeongezeka wakati muungnao huo wa kijeshi unakabiliana na vita vya Ukraine ambavyo ni vita shadidi zaidi barani Ulaya baada ya vita vikuu vya pili vya dunia.

Weledi wa mambo wanasema kuwa, NATO  ni tishio kubwa zaidi kwa usalama wa dunia kwa sababu muungano huo wa kijeshi unausukuma Umoja wa Ulaya ukabiliane kijeshi na Russia na China. Aidha wadadisi wa mambo wanakosoa uamuzi wa NATO wa kuzishinikiza nchi ambazo zilikuwa hazipendelei upande wowote kama vile Sweden na Finland kujiunga na muungnao huo wa kijeshi.

Hivi sasa inaelekea kuwa, baada ya Sweden na Finland kujiunga na NATO, taharuki baina ya Russia na muungano huo wa kijeshi zitaongezeka. Serikali ya Russia imekuwa ikionya mara kadhaa kuhusu kupanuka zaidi muungano wa kijeshi wa NATO.

Maria Zakharova Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema: "Wakati Vita Vikuu vya Pili vya Dunia vilipoanza, Hitler alizileta pamoja nchi kadhaa za Ulaya kukabiliana na kile alichodai kuwa ni 'tishio la Shirikisho la Sovieti' na leo pia NATO ikishirkiana na Umoja wa Ulaya zinatumia mbinu hiyo hiyo ya Hitler ya kuunda muungano wa kivita na mapambano dhidi ya Russia."

Kimsingi ni kuwa, NATO imevuruga usalama wa bara Ulaya  na kutokana na kupuuza indhari ya Russia, hivi sasa kutaibuka mashindano makubwa ya kijeshi, jambo ambalo litapelekea kuwepo hali ya taharuki na wasiwasi katika mipaka ya UIaya.

Rais Putin wa Russia

Rais Vladimir Putin wa Russia ameonya kuwa, katika kipindi cha miezi michache ijayo atapeleka nchini Belaruss mfumo mpya wa makombora ya balistiki ya Iskander-M. Mfumo huu unaweza kutumia makombora ya nyuklia ya balisitiki na ya kruz na hivyo hatua hiyo inathatminiwa kuwa ni ulipizaji kisasi wa Russia kwa hatua ya kichochezi ya NATO kujipanua zaidi upande wa mashariki.

Ingawa bado Sweden na Finland hazijajiunga na NATO, lakini inaelekea kuwa uamuzi wa NATO kujipanua na kupuuza mistari myekundu ya Russia ni jambo linaloweza kupelekea kushadidi vita vya kieneo ambavyo yamkini vikaenea kote duniani.

Tags