Jul 01, 2022 01:03 UTC
  • Sputnik: Marekani inawasajili magaidi wa Daesh ili kuwatuma Ukraine

Shirika la habari la Sputnik limeripoti kuwa, Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) linawasajili magaidi wa Daesh (ISIS) ili wapelekwe Ukraine kwa kisingizio cha vita nchini humo.

Sputnik imeripoti kuwa, shirika la ujasusi la CIA linasajili magaidi wa ISIS katika magereza au maficho yao eneo la Asia Magharibi ili kuwapeleka kupigana Ukraine kama mamluki.

Ripoti hiyo inakuja wakati Idara ya Usalama wa Nje ya Nchi ya Russia- SVR RF- imefichua kuwa, Marekani inawasafirisha magaidi wa ISIS au Daesh kutoka Syria na kuwaingiza Ukraine.

Taarifa ya SVR-RF imesema magaidi hao wa ISIS wamekuwa wakipata mafunzo maalumu katika kituo kimoja cha kijeshi kilicho Syria kinyume cha sheria na baada ya kupata mafunzo wanaepelekwa Ukraine.

Taarifa hiyo imesema: "Mwishoni mwa mwaka 2021, Marekani iliwaachilia huru wafungwa wakiwemo makumi ya magaidi wa ISIS, na miongoni mwao walikiwemo raia wa Russia na nchi za CIS. Watu hawa walipelekwa katika kituo cha kijeshi cha al Tanf kinachosimamiwa na Marekani ambapo wamepewa mafunzo maalumu ya mbinu za kigaidi za vita na wametumwa eneo la Donbass."

Idara ya Usalama wa Nje ya Nchi ya Russia imesema tayari magaidi wengi waliotumwa Ukraine wameshauawa katika operesheni maalumu ya jeshi la Russia nchini humo.

Vilevile mwezi Machi mwaka huu Wizara ya Ulinzi ya Russia ilitangaza kuwa Idara ya Ujasusi ya Jeshi la Marekani imeanzisha kampeni ya kuwaajiri mamluki ili kuiwapeleka vitani dhidii ya Russia. Imedokezwa kuwa mamluki wa mashirika ya American PMCs Academi, Cubic na Dyn Corporation wanapelekwa vitani Ukraine. Taarifa hiyo imesema wiki mwezi Machi pekee mamluki 200 kutoka Croatia waliwasili Ukraine kupitia Poland.

Rais wa Russia, Vladimir Putin tarehe 24 Februari aliamuru operesheni maalumu ya kijeshi katika eneo la Donbass kujibu ombi la msaada wa kijeshi kutoka kwa viongozi wa jamhuri za Donetsk na Luhansk huko Mashariki mwa Ukraine. Russia imekuwa ikilalamika kwa muda mrefu kuwa, serikali yenye misimamo ya Kimagharibi ya Ukraine inalenga kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO unaoongozwa na Marekani na hilo ni tishio kubwa kwa usalama wake.

Tags