Jul 01, 2022 08:02 UTC
  • Rais wa Russia atoa jibu zito kwa maneno ya upuuzi ya waziri mkuu wa Uingereza

Rais Vladimir Putin wa Russia amejibu kauli za kipuuzi na upayukaji za waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson alizotoa dhidi yake pembeni ya mkutano wa nchi wanachama wa G7.

Akimjibu Johnson aliyedai kwamba kama yeye Putin angelikuwa mwanamke katu asingeishambulia kijeshi Ukraine, rais huyo wa Russia amemkumbusha waziri mkuu wa Uingereza kuwa, shambulio la kijeshi la nchi hiyo dhidi ya visiwa vya Falkland lilifanywa katika kipindi cha uwaziri mkuu wa Bi Margaret Thatcher.

Putin amesema: "Ninataka nikumbushe baadhi ya matukio katika historia ya zama hizi; ni wakati Margaret Thatcher alipoamua kuanzisha operesheni za kijeshi dhidi ya Argentina katika visiwa vya Falkland. Kwa hiyo ni mwanamke ambaye alichukua uamuzi kutekeleza operesheni ya kijeshi."

Margaret Thatcher

Rais wa Russia ameongezea kwa kusema: "kwa hiyo waziri mkuu wa Uingereza hajahusisha kwa usahihi kamili kuhusu yanayoendelea kujiri hii leo. Visiwa vya Falkland viko wapi na Uingereza iko sehemu gani ya dunia? Hatua za Thatcher hazikuwa kitu kingine isipokuwa upendaji jaha wa kibeberu na hamu ya kuithibitisha nafasi ya kibeberu".../

 

 

Tags