Jul 02, 2022 03:00 UTC
  • Ukraine yalaumiwa kwa kutumia wanawake kama ngao ya vita

Wanajeshi wa Ukraine wanawatumia wanawake kama ngao za binadamu katika maeneo mbalimbali ya vita.

Ripoti zinasema, wakati maisha ya kawaida yakianza kurejea katika maeneo ya Donbas, baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamefichua na kutoa maelezo mapya kuhusu jinsi jeshi la Ukraine linavyotumia binaadamu, hasa wanawake, kama ngao za kujikinga na vita.

Wakazi wa maeneo hayo wamesema kuwa wanajeshi wa Ukraine wanawaweka mbele yao raia wakiwemo wanawake na kuwafyatulia risasi wanajeshi wa Russia. 

Wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakisimulia mengi kuhusu mienendo ya wanajeshi wa Ukraine na jinsi wanavyowatumia raia kama ngao za kujikinga na vita katika maeneo ya makabiliano yao na wanajeshi wa Russia. 

Rais wa Russia, Vladimir Putin tarehe 24 Februari aliamuru operesheni maalumu ya kijeshi katika eneo la Donbas kujibu ombi la msaada wa kijeshi kutoka kwa viongozi wa jamhuri za Donetsk na Luhansk huko Mashariki mwa Ukraine. Russia imekuwa ikilalamika kwa muda mrefu kuwa, serikali yenye misimamo ya Kimagharibi ya Ukraine inalenga kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO unaoongozwa na Marekani na hilo ni tishio kubwa kwa usalama wake.

Ukraine

Wakati huo huo, Samuel Werberg, msemaji wa kikanda wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ametangaza kuwa Washington itaendelea kutoa msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine kwa uratibu na washirika wake katika Umoja wa Ulaya na NATO.

Itakumbukwa pia kwamba, mapema mwezi uliopita, Rais Vladimir Putin wa Russia alionya kwamba nchi yake inaweza kuanza kupanua wigo wa mashambulizi yake nchini Ukraine ikiwa Magharibi itaimarisha misaada yake ya silaha kwa Ukraine ambayo zamani ilikuwa sehemu ya Shirikisho la Sovieti.