Jul 02, 2022 03:00 UTC
  • Lancet: Yumkini virusi vya Covid-19 vilitokea katika maabara Marekani

Jarida mashuhuri la masuala ya tiba na afya la The Lancet limesema virusi hatari vya Corona ambavyo vimeshaua mamilioni ya watu kote duniani vilizalishwa kwenye maabara, na wala havikuanza tu peke yake.

Jeffrey Sachs, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Covid-19 katika shirika la Lancet amesema, "Kwa mtazamo wangu, Covid-19 haikutoka katika hifadhi fulani asilia, bali ilitoka katika maabara ya bayoteknolojia ya Marekani kimakosa."

Amesema kuna ushahidi na ithibati nyingi zinazoonesha kuwa virusi vya Corona vilitoka kwenye maabara ya bayoteknolojia ya US, na kwa hiyo, haipaswi kusemwa kuwa virusi hivyo vilienea kwa ajali, bali vilienea kutokana na makosa na uzembe wa wahusika.

Katika miezi ya kwanza ya janga la Corona, aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump na viongozi wengine wa serikali ya Washongton walieneza propaganda kubwa wakidai kwamba kirusi cha Corona kimetengenezwa katika maabara ya mji wa Wuhan nchini China.

Soko la samaki la  Wuhan, China ambako Corona iliripotiwa kuanzia

Hata hivyo viongozi wa China walikanusha vikali madai hayo wakisisitiza kuwa ni uongo na hayana ushahidi wowote. Aidha Josep Borrell, Mkuu wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya alinukuliwa mara kadhaa akisema kuwa, madai hayo ya Trump kwamba asili ya kirusi cha Corona ni maabara ya Wuhan, China, si sahihi.

Huko nyuma pia, Philip Giraldi, mtaalamu wa zamani wa vita dhidi ya ugaidi ambaye pia alikuwa afisa wa kiintelijensia wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA alisema virusi hivyo vilizalishwa kwenye maabara, kwa lengo la kutumika kama kemikali ya vita vya kibayolojia.

Tags