Jul 03, 2022 07:53 UTC
  • Mbunge Marekani alaani nchi hiyo kujiingiza katika vita Ukraine kuvuna faida

Mjumbe mwanamke wa chama cha Republican katika Kongresi ya Marekani amekosoa vikali hatua ya Washington ya kuipa Ukraine msaada mkubwa wa kijeshi na kuisaidia nchi hiyo katika kile alichokiita vita vya niaba dhidi ya Russia.

Mbunge huyo wa Georgia, Marjorie Taylor Greene amesema hayo katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na kueleza kuwa: Wamarekani hawataki vita na Russia, lakini NATO na viongozi wetu wapumbavu wanatusukuma kwenye vita hivyo. Tunapaswa kujiondoa kwenye muungano wa NATO.

Mwanasiasa huyo wa chama cha Republican amesisitiza kuwa, "watu pekee wanaochechea moto wa mgogoro dhidi ya Russia ni wale ambao wanatengeza pesa (kupata faidi) kutokana na mgogoro wenyewe." 

Mbunge huyo wa Georgia amesema wanaofaidika na mgogoro wa Ukraine na Russia nchini Marekani ni Asasi Zisizo za Kiserikali, wenye kufunga mikataba ya kiulinzi ya kila aina, wajasiriamali, washauri wa kisiasa na hata mashirika ya misaada ya kibinadamu.

Silaha Ukraine

Amesema kimsingi, Wamarekani ambao wanalipa ushuru ndio wanaoifadhili bajeti yote ya ulinzi ya Ulaya, katika hali ambayo Ukraine si mwanachama wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO).

Nchi za Magharibi hasa Marekani zinaipatia Ukraine silaha na zana mbalimbali za kijeshi na kuzidisha mashinikizo kwa Russia tangu kuanza vita huko Ukraine, huku vita na mzozo vikishaididi ndani ya Ukraine. Ni zaidi ya miezi minne sasa ambapo Ukraine imeathiriwa na vita ambavyo Russia ilivianzisha lengo likiwa ni kuipokonya silaha Kiev na kujibu ombi la viongozi wa maeneo ya Donetsk na Luhansk. 

Tags