Jul 05, 2022 01:00 UTC
  • Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Ujerumani latahadharisha: Kukatwa gesi asilia ya Russia kutalemaza viwanda vikubwa

Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Ujerumani ametahadharisha kuwa tetesi za kuwepo uwezekano wa kukatwa gesi asilia ya Russia kwa ajili ya Ujerumani zitalemaza viwanda vikubwa nchini humo.

Bi Yasmin Fahimi anayeoongoza Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Ujerumani amesema kuwa, sekta nzima ya viwanda kama ile ya uzalishaji wa aluminiumu, vioo na viwanda vya kemikali iko katika hatari ya kuporomoka kwa sababu ya vikwazo dhidi ya Russia. Yasmin Fahimi ametoa tahadhari hiyo siku mbili kabla ya kukutana katika mazungumzo ya vuta nikuvute na Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz. 

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz 

Amebainisha kuwa mporomoko na mdororo wa sekta ya viwanda nchini Ujerumani utakuwa na taathira kubwa kwa uchumi mzima na ajira nchini humo. Fahimi ametilia mkazo suala hilo huku akitahadharisha kuhusu hatari zinazoweza kuiathiri Ujerumani ambayo inategemea sana nishati kutoka Russia, iwapo Moscow itasitisha kuiuzia gesi kwa nchi hiyo kama inavyotarajiwa.

Wakati huo huo Kansela wa Ujerumani amewatolea wito watu wa nchi hiyo kushikamana kutokana na kupanda kwa gharama za maisha; tatizo linaloendelea kuzikumba nchi zote za Ulaya.

Tags