Jul 06, 2022 05:53 UTC
  • Sergei Shoigu
    Sergei Shoigu

Waziri wa Ulinzi wa Russia amesema kuwa, nchi za Magharibi zinaendelea kutuma silaha nchini Ukraine kwa kisingizio cha kurefusha vita na hadi sasa zimepeleka zaidi ya tani elfu 28 za silaha huko Ukraine.

Tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, nchi za Magharibi zimejiepusha kuingia vitani moja kwa moja dhidi ya Russia, lakini zimeendelea kuipatia Ukraine silaha, zana za kijeshi na nishati.

Russia imekuwa ikisema mara kwa mara kuwa kutumwa silaha za Magharibi nchini Ukraine kutarefusha mzozo huo na imeonya kwamba vikosi vya jeshi la Russia vinaweza kulenga silaha hizo.

Akihutubia mkutano wa maafisa wa jeshi jana Jumanne, Waziri wa Ulinzi wa Russia, Sergei Shoigu, alisema kutumwa silaha za nchi za Magharibi huko Ukraine kunazidisha mvutano na kuongeza kuwa, nyingi kati ya silaha hizi zinauzwa katika masoko ya magendo ya silaha. 

Hapo awali, mtandao wa habari wa Russia Today uliripoti kuwa kutumwa silaha hatari kutoka nchi za Magharibi kwenda Ukraine wakati huu wa  vita nchini humo kumesababisha kuundwa kwa masoko haramu ya ununuzi na uuzaji wa silaha.

Russia imezionya mara kwa mara nchi za Magharibi kuhusu kuipatia Ukraine silaha na kupuuza ukiukaji wa haki za binadamu na mashambulizi ya vikosi vya jeshi la Ukraine dhidi ya raia wenye asili ya Russia mashariki mwa Ukraine.

Tags