Jul 13, 2022 03:42 UTC
  • Uchunguzi: Jeshi la UK liliua makumi ya wafungwa wa Kiafghani

Uchunguzi uliofanywa na shirika la habari la BBC la Uingereza umefichua kuwa, askari wa nchi hiyo ya Ulaya waliwaua kwa kuwafyatulia risasi raia zaidi ya 50 wa Afghanistan, licha ya kuwa hawakuwa wamejizatiti kwa silaha.

Kipindi cha Panorama kilichorushwa hewani Jumanne usiku na televesheni ya BBC kimefichua nyaraka zenye ushahidi unaoonesha kuwa, wanajeshi wa UK waliokuwa katika kambi ya jeshi ya Nad-e Ali mjini Helmand nchini Afghanistan mwaka 2010/2011, waliwaua wafungwa na raia wengi wa Kiafghani ambao hawakuwa na silaha yoyote.

Maveterani wa kijeshi wa Uingereza wameiambia BBC kuwa, kikosi kimoja cha jeshi la UK kiliua raia 54 wa Afghanistan katika operesheni zao ndani ya miezi sita, na kisha kuweka silaha pambizoni mwa maiti zao ili kupotosha ukweli wa mambo.

Maveterani hao wamesema, "Makamanda wetu walituambia kuwa wangelitulinda iwapo uchunguzi wa wimbi la mauaji dhidi ya raia nchini Afghanistan ungeanzishwa."

Askari vamizi waliovyokuwa wanawadhalilisha raia wa Afghanistan kabla hawajatimuliwa

BBC imefichukua kwenye makala hiyo kuwa, Jenerali Sir Mark Carleton-Smith, aliyekuwa Mkuu wa Vikosi Maalumu vya Jeshi la Uingereza alifahamishwa kuhusu mauaji hayo ya kiholela ya raia wa Afghanistan, lakini alificha ushahidi hata baada ya uchunguzi wa jinai hizo kuanzishwa.

Marekani, Uingereza na nchi nyingine za Magharibi zilizivamia nchi kadhaa za Waislamu kama vile Syria, Iraq na Afghanistan kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kuua mamia ya maelfu ya raia wasio na hatia wa nchi hizo.

Tags