Jul 26, 2022 02:23 UTC
  • Warepublican wanaogopa mno Trump kugombea urais 2024 nchini Marekani

Ripoti mbalimbali zinaonesha kuwa, viongozi waandamizi wa chama cha Republican cha nchini Marekani wana wasiwasi mkubwa wa kugombea urais Donald Trump mwaka 2024 kutokana na kashfa nzito zinazomkabili.

Miongoni mwa kashfa kubwa zinazomkabili Donald Trump ni kuchochea wafuasi wake kuvamia jengo la Congress tarehe 6 Januari 2022 wakati mabaraza ya Wawakilishi na Sanate ya Marekani yalipokuwa kwenye kikao cha kupasisha ushindi wa rais wa hivi sasa wa Marekani, Joe Biden.

Kumeuundwa kamati maalumu ya Baraza la Wawakilishi la Marekani iitwayo Kamati ya Januari 6 ya kufuatilia kashfa ya Donalt Trump ya kuchochea wafuasi wake kuvamia jengo la Congress kupinga ushindi wa Joe Biden.

Wanajeshi wa Marekani walimiminwa kulinda jengo la Congress la Marekani baada ya kuvamiwa na wafuasi wa Donald Trump

 

Watu wasiopungua watano waliouawa na makumi ya wengine kujeruhiwa wakati wa uvamizi huo ambao ulikwamisha kikao cha mabaraza hayo mawili ya Congress ya Marekani kwa masaa kadhaa.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, wanachama wengi waandamizi wa chama cha Republican wana wasiwasi sana wa kurejea Donald Trump kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2024.

Dan Crenshaw mmoja wa wajumbe wa kamati ya uchunguzi ya wahafidhina wa chama cha Republican cha Marekani amesema kuwa, hadhani kwamba Trump anaweza kugombea tena na hata akijitokeza, haamini kuwa atapata nafasi ya kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi wa 2024.

Mbunge mwingine wa Republican kutoka jimbo la Dakota amesema, hata kama uchunguzi wa maoni unaonesha Trump anaongoza, lakini si mara zote matokeo hayo yanasema kweli.

Tags