Jul 26, 2022 11:19 UTC
  • Korea Kusini ina hofu juu ya jaribio la 7 la nyukia linalokaribia kufanywa na Korea Kaskazini

Korea Kusini imesema, si baidi kwa Korea Kaskazini kufanya jaribio la saba la nyuklia hapo kesho.

Korea Kaskazini hadi sasa imeshafanya majaribio sita ya nyuklia, na tangu wiki kadhaa nyuma Seoul imekuwa ikisisitiza kuwa upo uwezekano wa Pyongyang kufanya jaribio jengine la saba.

Wizara ya Korea Kusini inayohusika na kuziunganisha upya Korea mbili imetangaza leo kuwa, kuna uwezekano mkubwa sana wa Korea Kaskazini kufanya jaribio la nyuklia katika maadhimisho ya "Siku ya Ushindi" ambayo inasherehekewa kesho Jumatano tarehe 27 Julai.

Kesho Jumatano, Korea Kaskazini itaadhimisha mwaka wa 69 wa usitishaji vita kati ya Korea mbili uliotekelezwa mwaka 1953.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un (kati aliyevaa miwani) akitoka kukagua kombora la nyuklia

Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Lee Jong-sup ametangaza leo kuwa mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ni tishio kubwa na akasisitiza kwamba kwa mtazamo wake, Pyongyang imeshachukua hatua zote zinazohitajika kwa ajili ya kufanya jaribio la saba la nyukia na kwamba wakati wowote ule utekelezaji wa jaribio hilo utafanyika kwa amri ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.

Korea Kaskazini ilifanya jaribio lake la sita na la mwisho la silaha za atomiki Septemba 2017.../ 

Tags