Jul 28, 2022 02:23 UTC
  • Trump: Marekani imekuwa taifa ombamba

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amesema nchi hiyo imegeuka na kuwa 'taifa ombaomba' na kwamba hivi sasa nchi hiyo inakumbwa na wimbi la udhalilishaji wa kihistoria.

Trump amesema hayo mjini Washington DC katika hotuba yake mbele ya mkutano wa kujadili 'Ajenda ya Kwanza ya Marekani' ulioandaliwa na taasisi ya America First Policy Institute na kueleza bayana kuwa, utawala wa Rais Joe Biden na wakuu wa chama cha Democratic wamelipigisha magoti taifa la Marekani.

Trump ambaye alikuwa anaonekana kwa mara ya kwanza hadharani jijini Washington tangu akabidhi hatamu za uongozi mwaka 2021, amesema "Taifa letu linakumbwa na udhalili mmoja wa kihistoria baada ya mwingine katika uga wa kimataifa."

Amesema uhuru na haki za msingi zinatoweka taratibu nchini Marekani, huku mamilioni ya wahamiaji haramu wakimiminika nchini humo kinyume cha sheria.

Trump na Biden

Mwanasiasa huyo wa chama cha Republican amedai kuwa, vifo vimeongezeka kwa kiasi cha kutisha katika majiji yanayosimamiwa na Wademocrats.

Aidha katika hotuba yake hiyo, Trump amekosoa kile alichodai ni kufeli kwa sera za utawala wa Biden, kulikopelekea kupanda kwa mfumko wa bei hadi asilimia 9.1, kiwango cha juu ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika karibu miaka 50 iliyopita. 

Tags