Jul 28, 2022 11:23 UTC
  • Canada yasema: Kuomba msamaha kwa Papa hakutoshi

Serikali ya Canada imeashiria matukio ya miaka ya nyuma na kashfa za viongozi wa Kanisa Katoliki za kuwabaka na kuwanajisi watoto wadogo na kutangaza kuwa: Hatua ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis ya kuomba msamaha kwa vitendo hivyo viovu haitoshi.

 kugunduliwa makaburi ya halaiki na miili ya mamia ya watoto nchini Canada kumeibua kashfa ya mauaji yaliyofanywa dhidi ya wenyeji na ubaguzi wa rangi dhidi yao. Ukubwa wa janga hilo uliwapelekea wanaharakati wa mashirika ya kiraia ya Canada na viongozi wa kisiasa nje ya mipaka ya Canada kulalamikia vikali suala hilo kiasi kwamba Justin Trudeau, Waziri Mkuu wa nchi hiyo, alilazimika kukosoa uzembe uliofanywa na serikali ya nchi hiyo na pia kulibebesha Kanisa Katoliki dhima ya maangamizi hayo ya umati, na wakati huo huo kumtaka Papa wa kanisa hilo asafiri nchini humo ili kuwaomba msamaha jamaa na familia za wahanga wa mauaji hayo.

Katika safari yake ya Jumatatu iliyopita nchini Canada, Papa Francis aliomba msamaha kwa wazawa wa nchi hiyo kwa jukumu la Kanisa Katoliki katika shule ambazo watoto wa wakazi asili walinyanyaswa na kudhulumiwa. Hata hivyo serikali ya Canada imesema kuomba msamaha kwa Papa hakutoshi.

Msimamo huo wa serikali ya Ottawa umetangazwa wakati Papa akiwasili Quebec kwa ajili ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Justin Trudeau na maafisa wengine wa nchi hiyo

Kanisa Katoliki na Serikali ya Canada, wamechangia pakubwa katika unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto wa wenyeji na wakazi asili katika karne za hivi karibuni kwa kuanzisha na kusimamia mamia ya shule za watoto waliotenganishwa kwa nguvu na familia zao. 

Wenyeji wa Canada ndio walikuwa wakazi asilia wa ardhi hiyo kabla ya kugunduliwa Marekani kwenye karne ya 15 na bado wanaishi ndani ya mipaka ya Canada ya leo wakijumuisha makabila ya awali ya Inuit na Metis. 

Takwimu zinaonesha kuwa, Canada ina zaidi ya Wahindi Wekundu milioni moja na laki mbili, na jamii yao inaishi katika hali mbaya ikisumbuliwa na kiwango cha juu ya umaskini, kujiua na uraibu wa dawa za kulevya. 

Ripoti iliyotolewa mwaka 2018 na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa iliashiria vipengee vya kibaguzi vilivyoko katika “Sheria ya Wenyeji” (Aboriginal Law) nchini Canada. Ripoti hiyo imesema kuwa, Canada inapaswa kufuta vipengee hivyo vya kibaguzi. Sheria hiyo ilibuniwa mwaka 1876 kwa misingi ya ubaguzi.

Ripoti zimeifichua unyanyasaji wa kutisha wa kimwili, ubakaji, utapiamlo na unyama mwingine uliowapata watoto wengi anokadiriwa kufikia 150,000 waliohudhuria shule hizo, ambazo zilikuwa zikiendeshwa na makanisa ya Kikristo kwa niaba ya serikali ya Ottawa. 

Maelfu ya Wahindi Wekundu walitoweka katika shule za Kanisa Katopliki

Haya yote na licha ya kuwa, Canada imekuwa ikijigamba kuwa mtetezi wa haki za binadamu na daima imekuwa ikijitokeza katika majukwaa ya kimataifa kama Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kuzituhumu nchi inazopinga sera za kibeberu za Wamagharibi.