Aug 10, 2022 01:21 UTC
  • Medvedev: Rais wa Ukraine anafuata fikra za Adolf Hitler

Rais wa zamani wa Russia amesema fikra, mienendo na misimamo ya Rais wa Ukraine inafanana na ya mtawala wa zamani wa Ujerumani ya Manazi, Adolf Hitler.

Dmitry Medvedev ambaye ni Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia alisema hayo jana Jumanne akijibu bwabwaja za Volodymir Zelensky, Rais wa Ukraine ambaye ametoa mwito kwa nchi zote za Magharibi kuwapiga marufuku raia wote wa Russia.

Medvedev ameeleza bayana kuwa, Zelensky anatekeleza siasa zile zile za Adolf Hitler, kiongozi wa zamani wa Kinazi nchini Ujerumani, kwa kutaka kuadhibiwa wananchi wote wa Russia.

Zelensky amesema Warusi wote bila kujali misimamo na itikadi zao za kisiasa wanapaswa kufukuzwa katika nchi za Magharibi haraka iwezekanavyo, na nchi hizo pia zisiwapokee raia wengine kutoka Russia.

dolf Hitler, kiongozi wa zamani wa Kinazi nchini Ujerumani,

Rais huyo wa Ukraine amedai kuwa, wananchi wa Russia ndio walioiachagua serikali inayowaongoza, na kwa msingi huo wote kwa ujumla wanapaswa kubebeshwa dhima. Ameongeza kuwa, wananchi wote wa Russia wamenyamaza kimya na wala hawapingi misimamo na sera za serikali hiyo kama ya kuishambulia Ukraine.

Rais wa zamani wa Russia akijibu matamshi hayo amebainisha kuwa, misimamo hiyo ya Zelensky inashabihiana na ile iliyochukuliwa na Adolf Hitler katika Vita vya Pili vya Dunia ambavyo vilisababisha zaidi ya watu milioni mbili kuuawa.

Tags