Aug 10, 2022 11:21 UTC
  • Marekani yatiwa kiwewe na hatua ya Iran kurusha satalaiti anga za mbali

Marekani imeghadhabishwa na hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kurusha satalaiti katika anga za mbali kwa mafanikio, kwa kutumia roketi la Russia.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema katika taarifa kuwa, kitendo cha Russia cha kupanua uhusiano na ushirikiano na Iran kinapaswa kutazamwa na dunia kama tishio kubwa.

Maafisa wa Marekani wametiwa kiwewe na mafanikio hayo makubwa ya Iran katika teknlojia ya anga za mbali, licha ya kuwekewa vikwazo vikali na kuwa chini ya mashinikizo ya juu kabisa ya Washington.

Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia wa Iran, Issa Zarepour amesema leo Jumatano kuwa, satalaiti hiyo ya Kiirani ya Khayyam imeshapokea data mara nne kufikia sasa tangu iliporushwa katika anga za mbali jana Jumanne.

Waziri wa Habari na Mawasiliano na Teknolojia wa Iran, Issa Zarepour

Amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ushirikiano na Russia itaendelea kuzalisha satalaiti za aina hii, na kwamba mfanikio haya ni fahari kubwa kwa wataalamu wa nchi mbili hizi.

Habari zaidi zinasema kuwa, satalaiti hiyo iliyozalishwa na wataalamu wa Iran itakuwa inatuma picha safi zenye ubora wa juu mara nne kwa siku.

 

 

Tags