Aug 11, 2022 02:25 UTC
  • Ombi la rais wa Ukraine la kuadhibiwa kwa umati wananchi wa Russia; muendelezo wa siasa za Kizayuni

Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine ambaye hadi hivi karibuni alikuwa anadai kuwa Rais Vladimir Putin wa Russia ndiye aliyesababisha vita vya Ukraine, hivi sasa ameelekeza mashambulizi yake kwa wananchi wote wa Russia na ametaka adhabu ya umati itolewe dhidi yao.

Licha ya vikwazo vikubwa vilivyowekwa na nchi za Magharibi dhidi ya Russia, lakini bado Zelenskyy ameziomba nchi za hizo za Magharibi ziwawekee vikwazo vikali zaidi wananchi wote wa Russia akidai kuwa wananchi hao wanaunga mkono vita vya Ukraine. 

Akihojiwa na gazeti la Washington Post, rais huyo wa Ukraine amesema, wananchi wote wa Russia lazima watengwe hadi pale watakapobadilisha misimamo yao. Wananchi wa Russia wanasema vita hivyo havituhusu. Hatuwezi kubebesha lawama watu wote. Lakini wananchi hao ndio waliochagua serikali iliyoko madarakani na wala hawaipingi wala hawawalamikii viongozi wao, hivyo wote lazima watengwe. Kwa mtazamo wa Zelenskyy, hata wale Warussia ambao wameondoka nchini humo na ambao wanapinga siasa za serikali yao, wote nao lazima wawekewe vikwazo na watengwe.

Rais wa Ukraine, Zelenskyy Zionist, katika mkutano na Wazayuni

Matamshi hayo yanaonesha wazi jinsi rais huyo wa Ukraine alivyo na hamu ya kuadhibiwa kwa umati wananchi wote wa Russia bila ya kujali wapinzani na waungaji mkono wa vita. Siasa hizo kwa kweli ndizo zile zile zinazofuatwa na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unafanya jinai na ukatili mkubwa dhidi ya wananchi wa Palestina kwa kisingizio cha harakati za makundi ya mapambano kama HAMAS na Jihad al Islami. Kwa zaidi ya miaka 15 sasa utawala wa Kizayuni wa Israel unawatesa wananchi wa Ghaza kwa kuwazingira kila upande na kosa lao pekee kwa mtazamo wa Wazayuni ni wananchi hao wa Ghaza kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuichagua harakati ya HAMAS kuwaongoza.

Mbali na kuuzingira kila upande na kuufungia njia zote za kuingia na kutoka Ukanda wa Ghaza, angani, ardhini na majini, lakini pia mara kwa mara utawala wa Kizayuni unafanya mashambulio ya kikatili dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Ghaza kwa kisingizio hicho hicho cha kupambana na makundi ya mapambano ya Palestina. Msimamo mkali mno uliochukuliwa hivi sasa na rais wa Ukraine wa kutaka kuadhibiwa kwa umati wananchi wote wa Russia kwa kweli na kuwa ni sawa na msimamo huo wa Wazayuni, lakini pia unatokana na chuki zake kubwa rais huyo kwa wananchi wa Russia. Msimamo huo kwa hakika unatokana na misimamo ile ile wa kuchupa mipaka ya barani Ulaya ya kuchukuia na kupinga wageni maarufu kwa jina la fikra za unazi mamboleo zilizofuatwa na nduli Adolf Hitler wa Ujerumani.  Zelenskyy amedai kuwa, kama wananchi wa Russia hawalalamikii vita vya Russia nchini Ukraine, kimya chao kinaonesha kuridhika kwao hivyo inabidi waadhibiwe wote.

Dmitry Medvedev. Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia

 

Tab'an maneno hayo ya chuki ya rais wa Ukraine yamejibiwa vikali na viongozi wa Moscow. Dmitry Medvedev. Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia amejibu msimamo huo mkali wa Zelenskyy kwa kuandika: Adolf Hitler alikuwa mtu anayetumia fikra kama hizi za Zelenskyy dhidi ya watu wote. Je, hivi sasa kumebakia shaka na swali lolote jingine kuhusu uhakika wa viongozi wa Ukraine?

Russia imekuwa ikisema mara kwa mara kwamba viongozi wa serikali ya Ukraine ambao ni vibaraka wakubwa wa Magharibi wana fikra za Kinazi za Adolf Hitler na inachofanya Moscow katika operesheni yake maalumu ya kijeshi huko Ukraine ni kupambana na viongozi wa namna hiyo, kuipokonya silaha nchi hiyo na kuhakikisha haiwi tishio kwa usalama wa Russia. Huko nyuma pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia aliwahi kusema kuwa Adolf Hitler wa Ujerumani alikuwa na damu ya Kizayuni. Hivi sasa kumezuka mvutano baina ya Russia na utawala wa Kizayuni kutokana na uungaji mkono mkubwa wa Israel kwa viongozi wenye fikra za kinazi wa Ukraine.

Kiujumla ni kwamba matamshi ya rais wa Ukraine ya kutaka wananchi wote wa Russia waadhibiwe kwa umati kwa madai ya kutopinga vita vya Ukraine ni muendelezo wa siasa zile zile za Kizayuni na za magenge yenye misimamo mikali ya kitaifa na ya kuchukia wageni ya nchi za Magharibi na hilo linazidi kubainisha uhakika na dhati ya viongozi wa Ukraine ambao Russia hivi sasa inapambana nao kuwavunja nguvu.

Tags