Aug 12, 2022 02:27 UTC
  • China: Marekani inataka vita vya Ukraine vichukue muda mrefu bila ya kumalizika

Balozi wa China nchini Russia amesema kuwa, hatua ya Marekani ya kuendelea kumimina silaha huko Ukraine ni ushahidi tosha unaothibitisha kuwa hamu ya Washington ni kuona vita vya Ukraine vinachukua muda mrefu bila ya kumalizika.

Vita vya Ukraine vimeingia kwenye mwezi wake wa sita vikiendelea na athari zake zote mbaya za kisiasa, kijeshi, kiuchumi kijamii na hata kiutamaduni.

Shirika la habari la IRIB limemnukuu Zhang Hanhui, balozi wa China nchini Russia akisema hayo na kuongeza kuwa, Marekani ndiye mwanzishaji mkuu wa mgogoro wa Ukraine na ndiyo inayorefusha vita hivyo.

Pamoja na kwamba madhara ya vita vya Ukraine ni makubwa, lakini nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zinaendelea kuchochea vita hivyo kwa kuwapa silaha wanamgambo wa Ukraine na viongozi wa nchi hiyo ambao ni vibaraka wakkubwa wa Magharibi bila ya kujali maafa yanayopatikana.

Ukraine inateketea na ndio kwanza nchi za Magharibi zinazidi kuchochea moto

 

Tangu vilipoanza vita vya Ukraine tarehe 24 Februari mwaka huu hadi hivi sasa, nchi za Magharibi zimeiwekea Russia vikwazo vikubwa ambavyo havijawahi kuwekewa nchi hiyo katika historia yake vikiwemo hata vikwazo vya michezo. Si hayo tu lakini pia nchi hizo zinawapa wanamgambo wa Ukraine silaha za kila namna licha ya kutambua vyema kuwa, Ukraine na wananchi wake ndio wahanga wakuu wa vita hivyo.

Russia iliingia kijeshi nchini Ukraine baada ya kuombwa na viongozi wa majimbo ya Luhansk na Donetsk na baada ya serikali ya vibaraka wa magharibi ya Kyiv kufanya mashambulio ya kikatili dhidi ya wakazi wa majimbo hayo mawili.

Tags