Aug 12, 2022 12:14 UTC
  • Askari wanne wa India wauawa Kashmir inayokaliwa na India

Askari wanne wa India wameuawa katika eneo la Kashmir linalokaliwa na kudhibitiwa na nchi hiyo.

Duru za habari zimeripoti kuwa, askari watatu wa India waliuawa siku ya Alkhamisi katika shambulio lililofanywa na watu wenye silaha wasiojulikana.

Shirika la habari la IRIB limeripoti leo kuwa askari wanne wa jeshi la India akiwemo afisa mmoja wameuawa katika shambulio lililofanywa na watu wasiojulikana kwenye kambi ya jeshi la India iliyopo katika eneo la Rajuri, Kashmir inayokaliwa na India.

Washambuliaji wawili waliokuwa na silaha wameuawa pia katika shambulio na mapigano hayo.

 

Kabla ya hapo, vijana wanne Wakashmir waliuawa katika operesheni ya kijeshi iliyofanywa na kikosi cha jeshi la India katika eneo hilo linalodhibitiwa na New Delhi.

Eneo la Kashmir linalozozaniwa na India na Pakistan tangu zama za uhuru wa nchi hizo, mnamo mwaka 1947 liligawanywa baina ya nchi mbili, huku kila nchi ikidai umiliki wa ardhi yote ya eneo hilo.

Tangu miongo mitatu iliyopita, makundi yanayobeba silaha katika eneo la Kashmir wanapambana na askari wa India wakitaka eneo hilo liwe nchi huru au liunganishwe na Pakistan, takwa ambalo serikali ya India inapinga utekelezaji wake…/

 

 

Tags