Aug 13, 2022 01:31 UTC
  • Bloomberg: China ina uwezo wa kuteketeza kwa muda mfupi ndege 900 za kivita za Marekani

Jarida la Bloomberg linalochapishwa Marekani limeandika kuwa, endapo vitazuka vita baina ya Marekani na China kwa sababu ya Taiwan, Wachina wataweza kwa muda mfupi kuziangamiza ndege za kivita 900 za Marekani, yaani nusu ya uwezo wote wa kikosi cha anga cha nchi hiyo.

Bloomberg limeeleza katika ripoti yake kuwa, sambamba na mazoezi makubwa ya kijeshi inayofanya China katika eneo la maji yanayozunguka kisiwa cha Taiwan, likiwa ni jibu la nchi hiyo kwa safari aliyofanya Nancy Pelosi, spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani katika kisiwa hicho, timu moja ya wataalamu wa kijeshi wa Marekani katika kituo cha “mitaala ya kimataifa na kistratejia” kimetoa taswira ya kushabihisha hali ya vita halisi kati ya nchi mbili endapo vitatokea katika mwaka 2026 na kubainisha kuwa, hata kama Marekani na Taiwan zitaweza kuishinda China katika vita hivyo, lakini zitapata hasara kubwa mno.

Mark Cancian, mshauri mwandamizi wa kituo hicho amesema, sababu ya maafa na hasara kubwa ambayo Marekani itapata katika vita dhidi ya China katika eneo hilo ni kwamba ili kuusambaratisha uwezo wa kijeshi wa China Wamarekani watalazimika kukabiliana kwa karibu mno na vikosi vya nchi hiyo.

Mark Cancian

 

 Cancian amefafanua kuwa, kabla ya kuweza kuishinda China katika vita vya majini Marekani italazimika kutuma vikosi vya kushambulia manowari za kivita za nchi hiyo hasa za usaidizi wa vikosi vya nchi kavu. Afisa huyo wa zamani wa jeshi la Marekani ameongezea kwa kusema: “ili kupata picha sahihi ya hasara itakayopata Marekani inabidi mtambue kwamba, baada ya ushabihishaji wa vita tumebaini kuwa, katika vita vitakavyopiganwa kwa muda wa wiki nnne, Marekani  itapoteza zaidi ya ndege zake 900 za kivita; idadi ambayo ni sawa na nusu ya uwezo wake wote wa kikosi cha anga.

Hata hivyo makisio hayo hayakutathmini hasara ya kiuchumi itakayopata China kutokana na vita hivyo wala ya kibinadamu itakayopata Marekani na waitifaki wake…/

 

 

Tags