Aug 14, 2022 11:18 UTC
  • Vita vya Ukraine vyaongeza njaa Marekani, Biden alaumiwa

Televisheni ya Fox News ya nchini Marekani imesema kuwa, idadi ya Wamarekani wasiotimiza mlo mmoja kwa sikuk imeongezeka na idadi ya watu wanaokwenda kuomba chakula katika taasisi maalumu za misaada imeongezeka katika nchi hiyo ya Magharibi.

Televisheni hiyo imesema katika ripoti yake kuwa, idadi ya watu wanaohitajia msaada wa chakula imeongezeka sana na kwamba kiwango cha watu wanaorejea kwenye taasisi za kugawa misaada ya chakula kinaongezeka kila siku na kufikia hata asilimia 45 kwa siku moja.

Ugonjwa wa corona na siasa za rais wa hivi sasa wa Marekani kuhusu vita vya Ukraine, vimetajwa kuwa ndiyo sababu kubwa ya ongezeko la njaa nchini Marekani.

Eric Cupp, mkuu wa taasisi ya misaada ya chakula ya San Antonio amesema, sasa hivi hali ya njaa ni mbaya nchini Marekani. Taasisi za kugawa misaada ya chakula zimepungua kwa asilimia 20 hadi 30 huku watu wanaohitajia misaada ya chakula wakiongezeka kwa asilimia 10 hadi 50. 

Idadi ya watu wasiotimiza mlo wao wa siku imeongezeka sana nchini Marekani

 

Amsema, hali iliyoko Marekani hivi sasa inakumbusha hali mbaya ya kipindi cha kuongezeka mno vifo na maambukizi ya corona ambapo kulionekana foleni ndefu mno za watu wanaoomba chakula. Amesema, ingawa taasisi zao zinafanya juhudi kubwa za kugawa chakula, lakini zimezidiwa na ongezeko la watu wanohitajia misaada hiyo.

Mkuu huyo wa taasisi ya misaada ya chakula ya San Antonio ameilaumu serikali ya Joe Biden, na kusema kuwa rais huyo wa Marekani amedai ana mkakati wa kukomesha kabisa njaa nchini humo ifikapo mwaka 2030. Kwa kweli ni aibu kubwa kuona kwamba tumo katika mwaka 2022 lakini kuna watu wana njaa katika nchi hii ambayo ni tajiri zaidi duniani.