Aug 17, 2022 02:40 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine: Magharibi inangoja tusalimu amri kwa Russia

Waziri wa mambo ya nje ya Ukraine amesema lakini pasi na kuwataja mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Magharibi kwamba, baadhi ya nchi zinangoja Ukraine isalimu amri ili zitatue matatizo yao yote.

Dmytro Kuleba amefafanua kwa kusema, badala ya mawaziri wa mambo ya nje kuuliza, nini inapasa kifanyike ili ushindi upatikane haraka, wamekuwa wakiniuliza mara kadhaa katika mikutano na mazungumzo kwamba, mtaweza kuendelea kupambana mpaka lini?

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine ameongezea kwa kusema: "ufahamu wangu mimi ni kuwa, kila mtu anasubiri Ukraine isalimu amri ili matatizo yote yaweze kutatuka yenyewe."

 

Tarehe 24 Februari, Rais Vladimir Putin wa Russia alitoa amri ya kuishambulia kijeshi Ukraine kuitikia ombi la viongozi wa maeneo mawili ya Donetsk na Luhansk mashariki ya nchi hiyo, lakini akatangaza kuwa lengo la Moscow ni kuipokonya silaha tu Ukraine na si kuikalia ardhi ya nchi hiyo.

Hii ni katika hali ambayo, nchi za Magharibi na hasa Marekani na Uingereza zimechukua hatua ya kuiwekea Russia vikwazo vya kila aina sambamba na kuipatia Ukraine aina mbali mbali za silaha na zana za kivita ili kuizuia Kyiv isiketi kwenye meza ya mazungumzo ya suluhu na Russia na kushadidisha pia vita na mapigano nchini humo.../