Aug 17, 2022 06:53 UTC
  • Guterres kutembelea Ukraine kesho Alkhamisi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kukutana na marais wa Ukraine na Uturuki katika ziara yake ya kesho Alkhammisi nchini Ukraine.

Hayo yamethibitishwa na msemaji wa Umoja wa Mataifa ambaye amesema, katibu mkuu wa umoja huo, António Guterres kesho Alkhamisi ataelekea mjini Lviv, magharibi mwa Ukraine na kuonana na rais wa nchi hiyo, Volodymyr Zelenskyy na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kuzungumza nao masuala muhimu ya kimataifa.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema pia kuwa, siku ya Ijumaa, Guterres atatembelea bandari ya Odesa ya kusini mwa Ukraine. Bandari hiiyo ni moja ya bandari tatu zinazotumika kusafirisha nafaka nje ya Ukraine kupitia Bahari Nyeusi.

Vita nchini Ukraine vimesababisha hasara kubwa

 

Kabla ya hapo yaani tarehe 26 Aprili mwaka huu, Guterres aliitembelea Russia na kuonana na Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo na siku mbili baadaye yaani tarehe 28 mwezi huo wa Aprili alikwenda nchini Ukraine kuonana na rais wa nchi hiyo, Volodymyr Zelenskyy. Kabla ya kuelekea Russia na Ukraine mwezi huo wa Aprili, Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alitembelea kwanza Uturuki na kuonana na rais wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan.

Hayo yamejiri katika hali ambayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, amesema kuwa badala ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za \Magharibi kuuliza, nini kinapasa kifanyike ili ushindi wa Ukraine upatikane haraka, wamekuwa wakiniuliza mara kadhaa katika mikutano na mazungumzo kwamba, mtaweza kuendelea kupambana mpaka lini? Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine ameongezea kwa kusema: "ufahamu wangu mimi ni kuwa, kila mtu anasubiri Ukraine isalimu amri ili matatizo yote yaweze kutatuka yenyewe."

Tags