Aug 30, 2022 09:43 UTC
  • Russia: Marekani irejeshe fedha za Afghanistan zilizoibwa

Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa ameitaka Marekani izirejeshe fedha zilizoibiwa Afghanistan.

Vasily Nebenzya ametoa mwito huo alipohutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
 
Kwa mujibu wa shirika la habari la Russia TASS, mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kujadili suala la Afghanistan uligeuka uwanja wa utoaji tuhuma za ​​mwakilishi wa Russia katika umoja huo dhidi ya mwenzake wa Marekani Linda Thomas-Greenfield.
 
Kwa mujibu wa TASS hatua ya mwakilishi wa Marekani UN ya kuzishutumu Russia na China kwamba zimetoa msaada mdogo sana wa kifedha kwa ajili ya ujenzi mpya wa Afghanistan, ilifuatiwa na jibu na matamshi makali ya balozi mwenzake wa Russia katika umoja huo. 
 
Katika kikao hicho cha Baraza la Usalama, Nebenzia ameashiria vita vya miaka 20 vya ukaliaji kwa mabavu ardhi ya Afghanistan viivyoanzishwa na Marekani na washirika wake dhima wanayopaswa kubeba kwa uharibifu na uangamizaji wa miundombinu ya nchi hiyo.
Vasily Nebenzya

 

Mwakilishi wa Kudumu wa Urusi katika Umoja wa Mataifa ameongezea kwa kusema: "ni washirika wetu wa zamani wa Magharibi; hapana ni ninyi, ndio mnaopaswa kulipa gharama za makosa yenu; na kwa kuanzia, kuna ulazima wa kuzirejesha fedha walizoibiwa watu wa Afghanistan."
 
Nbenzia amesisitizia kwa kusema: "si kila kitu kinaweza kupimwa kwa pesa. Roho za watu zilizopotea wakati mlipoibebesha Afghanistan demokrasia ya kulazimisha haziwezi kupimwa kwa pesa, na pesa haiwezi kununua uaminifu wa watu wa Afghanistan, na inavyoonekana Marekani imepoteza kikamilifu uaminifu wa watu wa Afghanistan."
 
Matamshi hayo ya Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa kuhusu Afghanistan yametolewa katika hali ambayo Marekani na baadhi ya washirika wake walizuia fedha na mali za Afghanistan baada ya kundi la Taliban kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo.
 
Baada ya Taliban kuingia madarakani nchini Afghanistan mnamo Agosti 2021, Marekani ilianza kutekeleza sera ya uadui na uhasama dhidi ya kundi hilo. Washington ilizidisha vikwazo dhidi ya Afghanistan na kuzuia dola bilioni kumi ambazo ni mali za benki kuu ya nchi hiyo wakati Waafghani wanaatilika kwa umasikini na hali mbaya ya uchumi.../

Tags