Sep 22, 2022 02:06 UTC
  • Uchunguzi wa maoni: Nusu ya wananchi wa Russia hawaoni kuwepo tishio la kushambuliwa kijeshi nchi yao

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni huko Russia unaonyesha kuwa asilimia 50 ya wananchi wa Russia wanaamini kuwa hakuna kitisho chochote cha kushambuliwa kijeshi nchi hiyo.

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti wa Maoni ya Umma cha Russia yaliyochapishwa jana Jumatano yanaonyesha kuwa asilimia 41 ya wananchi nchini humo wanaamini kuwa hakuna tishio lolote la uwezekano wa kushambuliwa kijeshi nchi yao. Hii ni katika hali ambayo, asilimia 9 ya wananchi pia wanaamini kuwa ni vigumu kutoa maoni na mitazamo yao kuhusu suala hilo. Wakati huo huo asilimia 62 ya wananchi wa Russia wanaamini kuwa, Marekani ni chanzo na ndiyo inayoeneza vitisho vya kushambuliwa kijeshi Russia.  

Hii ni katika hali ambayo Rais Vladimir Putin wa Russia jana Jumatano alihutubia kwa njia ya televisheni kwa ajili ya majimbo ya mashariki mwa Ukraine na Donbass ambayo yanataka kuitisha kura ya maoni ili kujiunga na Russia ambapo alitangaza zoezi la uhamasishaji mdogo wa kijeshi. Rais Putin aidha amesisitiza kuwa: nchi za Magharibi zinafanya kila linalowezekana kuidhofisha, kuisambaratisha na kuiangamiza Russia. 

Rais Vladmir Putin wa Russia 

Rais Vladimir Putin amebainisha kuwa, mchakato huo wa uhamasishaji wa kijeshi na kuwaita raia jeshini ulipangwa kuanza jana Jumatano; na kwamba hotuba yake hiyo inahusu kulinda mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya Russia sambamba na kuunga mkono hamu ya wananchi wa Russia ya kujiamulia mustakbali wao.  

 

Tags