Sep 23, 2022 02:42 UTC
  • Russia yakariri uwezekano wa kutumia silaha za nyuklia

Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia ameeleza kuwa: silaha zote zilizopo katika maghala ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na silaha za kimkakati za nyuklia zinaweza kutumiwa katika kuyalinda maeneo ya ardhi zilizoungana na Russia.

Dmirty Medvedev jana alibainisha kuhusu uwezekano wa Russia kutumia silaha za nyuklia katika kulinda ameneo yaliyoungana na Russia baada ya kujitenga na Ukraine. Medvedev ameongeza kuwa: kura ya maoni iliyoratibiwa na viongozi wa Russia na wa maeneo yanayotaka kujitenga itafanyika katika sehemu kubwa ya ardhi ya Ukraine na hakuna kurudi nyuma katika suala hilo."  

Wanasiasa wa maeneo la Luhansk, Donetsk, Kherson and Zaporizhzhia ambayo kwa pamoja yanaunda asilimia 15 ya ardhi yote nzima ya Ukraine wamepanga kuendesha kura ya maoni kuanzia tarehe 23 hadi 27 mwezi huu wa Septemba ili kujiunga na Russia.  

Donetsk and Luhansk 

Medvedev amesema: pande za Magharibi na kiujumla raia wote wa nchi wanachama wa Muungano wa Nato wanapasa kutambua kuwa Russia imechagua njia yake."  Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama wa Taifa la Russia kabla ya kubainisha haya alieleza kuwa akiba ya  silaha za nyuklia iliyonayo Russia ni dhamana bora kwa jaili ya kuilinda na kuihami nchi hiyo.  

Hifadhi ya silaha za kimkakati za nyuklia za Russia  zimegawanywa kwa upande wa jeshi la anga, baharini na vikosi vya nchi kavu; na kwa mujibu wa ripoti ya mwaka huu ya The Bulletin of the Atomic Scientist hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu Russia ilikuwa na silaha zisizo za  kistratejia za nyuklia za kujilinda zipatazo 1,912; zikiwa ni pamoja na makombora ya anga kwa anga, makombora mengine na vichwa vya nyuklia vya kujihami.

Silaha zote hizo tajwa zimehifadhiwa katika kituo maalumu.