Sep 23, 2022 02:43 UTC

Mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa majeshi ya Iran, Russia na China yataendesha maneva ya pamoja ya kijeshi ya baharini.

Hafla ya gwaride la kikosi cha Shahrivar 31 cha vikosi vya ulinzi vya Iran kwa mnasaba wa maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka wa 42 wa Kujihami Kutakatifu ilifanyika Tehran katika Haram Tukufu ya Imam Khomeini (MA), mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu na katika miji mingine ya Iran kwa kuhuhuriwa na makanda na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali na jeshi.  

Meja Jenerali Mohammad Bagheri amesema pambizoni mwa hafla hiyo ya gwaride la vikosi vya ulinzi vya Iran kwa mnsasaba wa kuanza Wiki ya Kujihami Kutakatifu akijibu swali la mwandishi habari wa Iran Press kuhusu kufanyika maneva ya pamoja ya baharini kwa kuzishirikisha nchi tatu za Iran, Russia na China huko kaskazini mwa bahari ya Hindi katika msimu wa mapukutiko mwaka huu kwamba: kuna uwezekano Pakistan, Oman na nchi nyingine kadhaa zikashiriki katika maneva hiyo ya kijeshi ya baharini.

Meja Jenerali, Muhammad Bagheri 

Meja Jenerali Mohammad Bagheri ameongeza kusema kuwa: Wizara ya Ulinzi na vikosi vya ulinzi vimesaini hati nzuri za makubaliano na nchi mbalimbali katika nyanja mbalimbali ikiwemo kubadilishana uzoefu, mafunzo, zana za kijeshi na kuendesha maneva za pamoja za kijeshi; masuala yanayoonyesha kupanuka ushirikiano na uhusiano wa kirafiki kati ya Iran na nchi za kanda hii na nyingine duniani. 

 

Tags