Sep 24, 2022 02:56 UTC
  • Russia: Silaha zote za NATO haziwezi kukabiliana na kombora letu la Sarmat

Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Makombora cha Russia amezungumzia teknolojia ya hali ya juu iliyotumiwa kutengenezea kombora la balestiki la kuvuuka mabara la Sarmat na kusisitiza kuwa, silaha zote za NATO haziwezi kukabiliana na kombora hilo.

Ikumbukwe kuwa vita vya Russia nchini Ukraine vilianza tarehe 24 Februari mwaka huu. Vita hivyo vilianza kwa uchochezi wa nchi za Ulaya na Marekani hasa baada ya Ukraine kutaka kujiunga na jeshi la nchi za Magharibi NATO ili vikosi vya jeshi hilo vijizatiti katika mipaka ya Russia.

Moscow inasema mara kwa mara kuwa, lengo lake si kuikalia kwa mabavu Ukraine bali ni kuwapokonya silaha viongozi wa serikali yenye fikra za kinazi na kizayuni ya Kyiv na kuzuia nchi za Magharibi na Marekani kujizatiti kijeshi kwenye mipaka yake.

Ukraine imeteketezwa vibaya na vita vilivyochochewa na nchi za Magharibi

 

Nchi za Ulaya na Marekani lakini zimeiwekea Russia vikwazo vikubwa mno ambavyo havijawahi kuwekwa katika historia yote ya nchi hiyo kwa kisingizio cha vita vya Ukraine. Aidha nchi hizo Magharibi zinaendelea kumimina silaha zao kubwa na ndogo nchini Ukraine kwa ajili ya kukabiliana na Russia. Mara kwa mara Moscow inasema, haipigani na Ukraine tu, bali inapigana na nchi zote za Magharibi.

Kuhusu kombara la Sarmat, televisheni ya Al Jazeera ya Qatar imemnukuu Vladimir Degtyar, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Makombora cha Russia akisema, kombora la Sarmat la nchi hiyo linatumia teknolojia ya hali ya juu na hakuna silaha yoyote ya NATO inayoweza kukabiliana nalo.

Kombora hilo la Russia lina kasi zaidi ya sauti, lina uzito wa tani 100, linaweza kupiga sehemu yoyote ile duniani, lina uwezo wa kubeba kichwa cha tani 10 na kwenda kwa kasi ya kilomia 11,000 kwa saa. Lilifanyiwa majaribio kwa mafanikio miaka minne iliyopita.