Sep 26, 2022 11:36 UTC
  • Mikrofoni yamnasa rais wa Korea Kusini akiwatusi wabunge wa US kwa kuwaita

Rais Yoon Suk-yeol wa Korea Kusini amesema ripoti za vyombo vya habari kuhusu matamshi aliyotoa wakati wa safari yake mjini New York, si sahihi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Rais wa Korea Kusini amesikika katika mkanda wa video akiwaita wabunge wa Marekani "wapumbavu" na kusema, wanaweza kumwaibisha rais wa wa nchi hiyo Joe Biden kwa kutoidhinisha ufadhili wa fedha kwa ajili ya mipango ya afya duniani.
Tarjumi nyingine iliyotolewa na televisheni ya MBC ya Marekani inadai, rais wa Korea Kusini alisema: 
"Ikiwa wanaharamu hawa katika bunge hawataidhinisha, maskini (Rais wa Marekani Joe) Biden ataonekana mbaya sana."
Katika mkutano wake wa hivi karibuni na rais wa Korea Kusini, Joe Biden alimuahidi Yoon Suk-yeol kwamba serikali ya Marekani, ikiwa itaidhinishiwa na bunge la nchi hiyo, itachangia dola bilioni 6 kwa operesheni za kimataifa za kupambana na ukimwi, malaria na kifua kikuu.
Biden (kushoto) na Yoon Suk-yeol (kati)

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Rais wa Korea Kusini Yoon Suk-yol alisema kuwa, taarifa za uwongo za vyombo vya habari kuhusu matamshi yake pembeni ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa zilipangwa kuharibu uhusiano kati ya Seoul na Washington.

Ofisi ya rais wa Korea Kusini imejaribu kudhibiti suala hilo kwa kusema kwamba Yoon hakuwa akimaanisha viongozi waliochaguliwa wa Marekani.
Msemaji wa serikali ya Korea Kusini amesema, Yoon Seok-yul hakumtaja Biden kwa jina na kwamba neno alilotumia pengine linafanana kifonetiki na Biden.
Lakini mkuu wa chama cha upinzani nchini Korea Kusini cha kidemokrasia amesema, hoja zilizotolewa na ofisi ya rais hazina msingi na kwamba wanachofanya viongozi wa Seoul ni kujaribu kujinasua kwenye kinamasi cha janga la kidiplomasia.
Hayo yamejiri huku ripoti kutoka nchini Korea Kusini zikieleza kwamba umashuhuri wa Yoon Suk-yol umeanza kupungua tangu lilipoibuka sakata hilo lililojiri siku ya Jumatatu iliyopita.../

Tags